Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akipewa zawadi ya fimbo mara baada ya kuvishwa vazi aina ya kikoi ikiwa ni ishara ya kumpongeza kwa utendaji kazi wake mzuri katika masuala ya Uhifadhi wa Wanyamapori wakati wa mkutano kati ya Wenyeviti wa Muungano wa Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori nchini (WMAs) na Wizara ya Maliasili na Utalii uliofanyika leo jijini Dodoma.

TUTAFANYA MAGEUZI KWENYE JUMUIYA ZA HIFADHI ZA WANYAMAPORI – NAIBU WAZIRI KANYASU

K
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na Wenyeviti wa Muungano wa Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori nchini (WMAs) kwenye mkutano wa siku moja uliolenga kuimarisha ushirikiano kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Wadau wa uhifadhi wa Wanyamapori nchini uliofanyika  jijini Dodoma.
  • Serikali imewahakikishia Wenyeviti wa Muungano wa Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori nchini (WMAs) kuwa itaendelea kufanya mageuzi pamoja na kuwapa ushirikiano kwa kuendeleza dhana halisi ya uhifadhi wa wanyamapori shirikishi katika jamii.
K
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na nNyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa mara baada ya kuwasili kwenye mkutano wa Wenyeviti wa Muungano wa Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori nchini (WMAs) wa siku moja uliolenga kuimarisha ushirikiano kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Wadau wa uhifadhi wa Wanyamapori nchini uliofanyika  jijini Dodoma. SWengine ni watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Wafanyakazi wa WWF.
  • Hayo yamebainishwa  jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Constantine Kanyasu wakati akizungumza na wenyeviti hao kwenye mkutano wa siku moja uliolenga kuimarisha ushirikiano kati ya wizara na wadau hao wa uhifadhi nchini.
  • Amesema Wizara itaendelea kutatua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo kwa kuwa inatambua mchango mkubwa wanaoutoa katika shughuli za uhifadhi wa wanyamapori nchini.
  • Aidha, Mhe. Kanyasu ameziagiza WMAs zinazotegemea kufanya uchaguzi hivi karibuni ziendelee na utaratibu wa zamani wa kutumia kigezo cha elimu ya kuanzia darasa la 7 na kuendelea.
K
Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya za Hufadhi za Wanyamapori, George Wambura akizungumza na Wenyeviti wa Muungano wa Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori nchini (WMAs) kwenye mkutano wa siku moja uliolenga kuimarisha ushirikiano kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Wadau wa uhifadhi wa Wanyamapori nchini uliofanyika jijini Dodoma.
  • Amesema lengo la  kuruhusu kutumika kwa kigezo hicho cha elimu  ya darasa la saba na kuendelea ni kutoa fursa kwa  wagombea wengi wenye uwezo kuweza kujitokeza.
  • Amezitaka WMAs hizo  kuchagua viongozi watakaokua na uwezo wa  kutekeleza  mipango mbalimbali kwa ufanisi.
K
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati) akiwa na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii wa mkutano wa Wenyeviti wa Muungano wa Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori nchini (WMAs).
  • Hata hivyo, amesema kuwa yapo baadhi ya mambo ya msingi ambayo Wizara imeanza kuyaboresha kwenye kanuni za WMAs  likiwemo suala la kiwango cha elimu kwa viongozi wa WMAs nchini ili kupunguza migogoro isiyo ya lazima inayojitokeza mara kwa mara ndani ya WMAs hizo.
  • Kwa upande Mwenyekiti wa Muungano huo, Bw. Christopher Mademula amemueleza Mhe.Kanyasu kuwa suala la kigezo cha elimu liangaliwe kwa mapana yake kwa kigezo kuwa ikiwa wagombea wa darasa la saba hawataruhusiwa kugombea nafasi za uongozi kwenye WMAs, kitendo hicho kitachochea ujangili kwa kuwa wao wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa taarifa za kiinteligensia za ujangili kwenye maeneo yao
Ad

Unaweza kuangalia pia

SPIKA WA BUNGE AZINDUA JENGO LA MAHAKAMA WILAYA YA KONDOA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) leo azindua …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *