TAASISI ZA FEDHA ZATAKIWA KUCHANGAMKIA VIWANDA VYA USINDIKAJI MAZIWA

MI
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akizungumza jambo na Meneja Mwandamizi wa idara ya Kilimo biashara NMB Oscar Rwechungura pamoja na wafanyakazi wa NMB kwenye banda la benki hiyo wakati wa Wiki ya Maziwa kitaifa iliyofanyika jijini Arusha.
  • Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo,Profesa Elisante Ole Gabriel amezitaka taasisi za fedha nchini kuchangamkia fursa ya soko la usindikaji wa maziwa ambalo linahitaji uwekezaji wa kimkakati kutokana na sehemu ndogo ya maziwa yanayotoka kwa wafugaji ndiyo yanayosindikwa.
  • Profesa Ole Gabriel ametoa rai hiyo katika kongamano la 10 la Wiki ya Maziwa kitaifa nchini kuwa kiwango cha maziwa kwa mwaka ni takribani lita 2.7 bilioni wakati kiwango cha maziwa kinachosindikwa ni lita 56 milioni pekee hatua inayomnyima mapato mazuri mfugaji.
MI
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akizungumza jambo na Meneja Mwandamizi wa idara ya Kilimo biashara NMB Oscar Rwechungura pamoja na wafanyakazi wa NMB kwenye banda la benki hiyo wakati wa Wiki ya Maziwa kitaifa iliyofanyika jijini Arusha.
  • “Nitoe wito kwa taasisi za fedha kuchukua fursa hii muhimu kwa kuwekeza kwa nguvu kwenye mnyonyoro wa thamani ili kuyapa thamani maziwa yetu,ipo fursa kubwa ambayo itawasaidia wafugaji na taasisi zenu kupata faidi,”alisema Ole Gabriel
  • Kongamano hilo limewaleta wadau kutoka mikoa mbalimbali na nje ya nchi linajadili namna ya kuongeza uzalishaji bora wa maziwa na namna ya kukabiliana na changamoto za upatikanaji wa mbegu bora za uhamilishaji,malisho ya mifugo,masoko ya maziwa na uhaba wa viwanda vya usindikaji wa maziwa.

MI

  • Mweneyekiti wa Bodi ya Maziwa nchini,Lucas Malunde alisema viwanda zaidi vinahitajika kwaajili ya kuongeza kiwango cha maziwa yaliyosindikwa ambayo yanamhakikishia faida mfugaji na mtumiaji wa maziwa.
  • Alisema kiwango cha matumizi ya maziwa kwa mtu mmoja hapa nchini kipo chini kiasi cha lita 49 kwa mwaka wakati lengo ni kumwezesha kila mtu kutumia lita 200 kwa mwaka.
  • Afisa Utafiti wa benki ya NMB, Mboka Mwanitu alisema benki hiyo imetenga kiasi cha Sh 500 bilioni “for AVC” na tasnia ya maziwa kwa ujumla na hadi sasa wapo wajasiriamali walionufaika kwa kuchukua mkopo wa Sh 30 bilioni na hii imetokana na kuongezeka kwa mahitaji ya maziwa nchini.
  • Alisema mikopo yao imejielekeza kwenye kupata mbegu bora za ng’ombe,kuwa na vituo bora vya kukusanyia maziwa ,vifaa vya kisasa vya usindikaji wa maziwa,malisho na huduma za chanjo na matibabu .
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA, ATEMBELEA CHUO CHA UVUVI KUNDUCHI, JIJINI DAR ES SALAAM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *