BAIDU KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII VYA TANZANIA NCHINI CHINA

UT 1-01
Wataalam wa Masula ya film wa kampuni ya Baidu kutoka China wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere Terminal III, kwa ajili ya kutembelea maeneo ya vivutio vya utalii Tanzania lengo likiwa ni kujionea na baadaye kuzalisha film na picha ya vivutio hivyo kwa ajili ya mtandao wa Baidu.

 

  • Katika Jitihada za kukuza utalii nchini Taasisi iliyopewa jukumu hilo yaani Bodi ya Utalii Tanzania(TTB) ikishirikiana na Ubalozi wa Tanzania Nchini China, wamewezesha kampuni ya Beijing Pseacher Business na Baidu kuja nchini kutembelea na badaye kufanya kazi ya uzalishaji wa picha mjongeo(Film) na picha zitakazowekwa kwenye mtando wao wenye wafuasi takribani 700 kwa lengo la kutangaza utalii wa Tanzania.
UT 2-01
Wataalam wa Masula ya film wa kampuni ya Baidu kutoka China wakipata maelezo kutoka kwa kiongozi wao Prof.Li Kunruonan, mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere Terminal III, wataalam hao wako nchini kwa siki 11 kutembelea maeneo ya vivutio vya utalii Tanzania lengo likiwa ni kujionea na baadaye kuzalisha film na picha ya vivutio hivyo kwa ajili ya mtandao wa Baidu.
  • Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Bodi ya Utalii, Geofrey Tengeneza alisema kuwa ujio wa wageni kutoka China ni neema kwa sekta ya utalii, kwani utawezesha kuwepo kwa mradi mkubwa wa kupiga picha na kutengeneza Film ya vivutio vya utalii Tanzania ambavyo vitatangazwa kwenye mtandao wa Baidu na kuwezesha watalii kutoka China kuja kutalii nchini
  • “Tumefanya kazi kubwa kwa kushirikiano na Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini China, ambapo tumepata kampuni hii waliowasili leo kutembelea na baadae kuja kufanya mradi wa kupiga picha, kutengeneza makala ya vivutio vyetu, vyakula vyetu vya asili, lakini pia watapata fursa ya kutembelea Serengeti, Bonde la Mamlaka ya Ngorongoro, Zanzibar na bagamoyo na badae watafanya mradi huo ambao utaisaidia Tanzania kuliteka soko la utalii la China”, Geofrey Tengeneza.
UT 4-01
Wacheza ngoma wa Kikundi cha Nimujo wakitoa burudani kwa wageni wa kampuni ya Baidu (hawapo pichani), mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere Terminal III leo Agosti 22, 2019.
  • Tengeneza alisema kuwa wataalam hao 12 kutoka Baidu wamekuja kwa lengo la kuona jinsi gani watafanya mradi huo mkubwa ili kuwezesha uzalishwaji Film, picha za kawaida na kuziweka kwenye mtandao wao ambao unawafuasi wengi na hii itasaidia kukuza soko la utalii wa Tanzania kwa upande wa soko la China.
  • Aliongeza kuwa leongo la TTB ni kuiwezesha sekta ya utalii kupata watalii wengi kutoka china na kuongeza idadi ya watalii wa kigeni wanakuja kuitembelea Tanzania kutokana na kuona vivutio vitakavyochukuliwa kwenye mradi huo wa kampuni ya Baidu.
UT 5-01
Mpiga ngoma wa Kikundi cha Nimujo akipiga ngoma kwa wageni wa kampuni ya Baidu (hawapo pichani), mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere Terminal III leo Agosti 22, 2019.
  • Kwa upande wake kiongozi wa kundi hilo, Prof. Li Kunrounan alisema kuwa wamekuja Tanzania ili kuona jinsi gani wataweza kutekeleza mradi huo wa uzalishaji wa film kubwa ya vivutio vya utalii Tanzania na kuiweka kwenye mtandao huo mkubwa ili kukuza ushirikiano wa Tanzania na China kwenye Sekta ya Utalii.
  • “tumekuja kujionea maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii nchini Tanzania na baada ya hapo tutakuja sasa kufanya film na picha ambazo tutaziweka kwenye mtandao wetu unafuatiliwa na watu zaidi ya milioni 700 nchini China”; alisema Prof. Li Kunrounan
  • Prof. Li Kunrounan alieleza kuwa Tanzania ina vivutio vingi sana ikiwemo wanyama, mabonde pamoja na fukwe mbaliambali hayo ni moja ya maeneo ambayo yanahitaji kuitangazwa, lakini pia watu wake ni wakarimu sana.Na. Paschal Dotto-MAELEZO
Ad

Unaweza kuangalia pia

ZANZIBAR NA ANGOLA KUSHIRIKIANA KWENYE SEKTA YA UTALII

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameupongeza uwamuzi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.