MRADI WA KUFUA UMEME WA MAJI JULIUS NYERERE KATIKA MAPOROMOKO YA MTO RUFIJI UNAOTEKELEZWA NA SERIKALI ULIASISIWA NA BABA WA TAIFA MWAKA 1975

  • Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya Tano inatekeleza kwa vitendo Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere katika Maporomoko ya Mto Rufiji unaojulikana kama Julius Nyerere HydroPower Project ambao uliasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere mnamo mwaka 1975.
JL 1-01
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisoma kitabu cha Tanzania News Review kinachoonyesha kuwa Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere katika Maporomoko ya Mto Rufiji unaojulikana kama Julius Nyerere HydroPower Project uliasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere mnamo mwaka 1975.
  • Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) mara baada kufanya ziara ya kikazi Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dar es Salaam na kujionea kitabu cha Tanzania News Review cha mwaka 1977 kinachoainisha kuwa, Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere ndiye Muasisi wa mradi huo.
  • Dkt. Mwanjelwa amesema, Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli imekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza masuala yenye maslahi kwa taifa yaliyoasisiwa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere.
JL 2-01
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisoma kitabu cha Tanzania News Review kinachoonyesha kuwa Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere katika Maporomoko ya Mto Rufiji unaojulikana kama Julius Nyerere HydroPower Project uliasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere mnamo mwaka 1975.IMG_5001 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akishuhudia baadhi ya nyaraka muhimu zinazotunzwa na Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa wakati wa ziara yake ya kikazi katika Idara hiyo jijini Dar es Salaam
  • “Hakika ule usemi wa zidumu fikra za Mwalimu Nyerere umetekelezwa kwa vitendo na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika ujenzi wa mradi huu,” amefafanua Dkt. Mwanjelwa.
  • Aidha, Dkt Mwanjelwa ameitaka Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa kuwa na utaratibu mzuri wa kuuhabarisha umma juu ya taarifa muhimu za kihistoria ambazo si za siri ili watanzania wajue maamuzi mbalimbali ya kizalendo yaliyofanywa na viongozi wao kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa.
JL 3-01
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akishuhudia baadhi ya nyaraka za Waasisi wa Taifa zilizotunzwa katika maktaba ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi katika Idara hiyo.
  • Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi amemhakikishia Dkt. Mwanjelwa kuwa Idara yake itaendelea kutunza vizuri na kwa uadilifu mkubwa nyaraka muhimu za nchi za kabla na baada ya uhuru kwani nyaraka hizo ni rejea muhimu katika utendaji kazi wa Serikali.
  • Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere katika Maporomoko ya Mto Rufiji unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2022 na utakuwa ukifua megawati 2,115 kwa siku.
Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS MAGUFULI AIPONGEZA MAHAKAMA NA WADAU KWA MAFANIKIO MAKUBWA

Rais  Dkt. John  Magufuli ameipongeza Mahakama na wadau wake kwa hatua kubwa za kimaendeleo zilizopigwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *