KITUO CHA GESI ASILIA CHA SONGAS CHATAKIWA KUWASILISHA MPANGO KAZI

 • Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mussa Sima ameagiza kituo cha kupokea gesi asilia cha Songas eneo la Somanga kuwasilisha mpango kazi wa usimamizi wa mazingira unaoonesha madhara na hatua zinazochukuliwa pindi yanapotokea maafa.
 • Sima alitoa agizo hilo jana wakati wa ziara yake akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Prof. Esnat Chagu na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Samuel Gwamaka kukagua kituo hicho ambacho hivi karibuni kilipata tatizo la kuvujisha bomba la gesi katika eneo hilo wilayani Kilwa mkoani Lindi.
4-01
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima (kulia) akitoa maelekezo baada ya kukagua kituo cha kupokea gesi asilia cha Songas.
 • Katika ziara hiyo inayohusisha mikoa ya Lindi na Mtwara alisema kuwa ni muhimu wananchi wa vijiji zaidi ya 60 vilivyopitiwa na mradi wa bomba la gesi asilia licha ya kujua faida zake lakini pia wanatakiwa wapate elimu sahihi ya madhara pindi yanapotokea matatizo kama haya.
 • Aidha, Naibu Waziri huyo aliongeza kuwa nchi yetu imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi na hasa ya gesi asilia na kutaka mikataba ambayo inaingia na wakandarasi lazima ioneshe wananchi wameshirikishwaje na kuelewa kuhusu madhara yatakajitokeza endapo gesi itavuja.
3-01
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai akizungumzia kuhusu tukio la kuvuja kwa gesi lilivyotokea mbele ya viongozi mbalimbali wakati wa ziara hiyo.
 • Alisema kuwa lazima kama nchi tujuie mikataba hii ili kama yakitokea maafa wao wanawajibikaje kutokana na madhara yanayoweza kujitokeza hususan kwa wananchi wanaopitiwa na miradi hiyo.
 • “Tumekuja hapa tuone kama miradi hii inafuata Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 na hapa tunataka tuone kwenye eneo hili yakitokea madhara ni hatua gani zinachukuliwa, tunataka kuona taarifa kamili na tuangalie kwenye eneo letu la mazingira mnachukua hatua gani.
2-01
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima (kulia) akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai mara baada ya kukagua kituo cha Songas.
 • “Hebu turudi kuangalia mkataba huu makubaliano gani tunawekeana sio valvu mpya imetoka maabara imekuja ikawekwa hapa halafu ikajivusha gesi, hapana lazima tuje na majibu sahihi. Natambua wizara husika imefanya kazi yao na sisi tunaoratibu shughuli za mzingira lazima tufanye kazi yetu,” alisema Sima.
 • Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya NEMC) Prof. Chagu alisema ni muhimu kwa watalamu kuhakikisha vifaa vinavyototumika vinakuwa na viwango.
 • Prof. Chagu alisema kuwa matumizi ya vifaa vyenye viwango yatasaidia katika kuhakikisha matatizo kama haya hayatokei na kuleta madhara kwa wananchi na hata kama yakitokea basi lazima tujue hatua za kuchukua.
1-01
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima (kulia) akiwasili katika kituo cha kupokea gesi asilia cha Songas eneo la Somanga Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi kwa ajili ya kukagua na kupokea taarifaya madhara yaliyotokana na kuvuka kwa nishati hiyo. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai.
 • Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai alisema hili ni tukio baya kutokea na kama wasingekuwa makini kuzuia cheche ingekuwa hali ya hatari na kusababisha maafa makubwa.
 • Ngubiaga alibainisha kuwa katika siku ya tukio hilo wananchi wanaotumia Barabara ya Kilwa hususan wasafiri wa mabasi ya kwenda au kutoka Mtwara na Songea waliathirika kutokana na kutoendelea na safari.
 • Pia alisema kuwa athari za kiuchumi zilionekana kutokana kuzimwa kwa kituo cha umeme Kilwa kutoka muda wa jioni hadi usiku hivyo wananchi walikosa huduma hiyo na kushindwa kufanya shughuli za kiuchumi. Na Robert Hokororo, Kilwa
Ad

Unaweza kuangalia pia

TANZANIA YATAKA AMANI KUPUNGUZA MZIGO WA WAKIMBIZI AFRIKA

Tanzania imetaka Umoja wa Afrika na Jumuiya za Kimataifa kuongeza jitihada na nguvu katika kuleta …

8 Maoni

 1. Узнай все о недвижимости на одном ресурсе! Наши интересные статьи о квартирах от застройщика и о агентствах недвижимости помогут тебе разобраться во всех нюансах этой сложной сферы.
  Не упусти возможность быть в курсе всех изменений и принимать взвешенные решения! Посети наш сайт и стань экспертом в области продажи недвижимости!

 2. Портал о культуре – ваш гид по культурной жизни города. Здесь вы найдёте информацию о театрах, музеях, галереях и исторических достопримечательностях. Откройте для себя яркие события, фестивали и выставки, которые делают Ярославль культурной жемчужиной России.

 3. На нашем сайте вы найдете полезные статьи, которые помогут вам разобраться во всех вопросах покупки недвижимости.
  Вас ждут статьи на такие темы, как ремонт в новостройке, а также аренда офиса, и многие другие!

 4. Читайте информационные статьи на интересные темы, связанные с покупкой недвижимости, например квартира от застройщика или налог на недвижимость.

 5. Читайте интересные статьи на важные темы, связанные с недвижимостью, например квартиры в ЖК или продажа недвижимости.

 6. Интересуетесь недвижимостью? Наш портал – ваш верный проводник в этой области. Здесь вы найдете множество актуальных статей на такие темы, как квартиры в новостройке от застройщика, а также приемка квартир без отделки.
  Подробные аналитические материалы, экспертные мнения и простые рекомендации — все это доступно у нас!

 7. Хотите стать счастливым обладателем собственной недвижимости, но не знаете, с чего начать?
  Наш ресурс предлагает вам полную информацию на такие темы, как ремонт в новостройке или услуги риэлтора.

 8. Хотите быть в курсе всех новых тенденций на рынке недвижимости?
  На нашем сайте вы найдете информационные статьи на такие темы, как жилая недвижимость, а также прописка в новостройке.
  Узнавайте первыми о самых актуальных предложениях и важных советах от экспертов!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *