NITAENDELEA KUONGEA KWA NAMBA (TAKWIMU) BADALA YA MANENO – WAZIRI WA MADINI DOTO BITEKO

  • Waziri wa Madini Doto Biteko amesema ataendelea kuongea kwa namba (takwimu) badala ya maneno huku akiongeza kuwa wizara yake itavuka malengo ya makadirio ya makusanyo ya fedha zilizopangiwa na wizara yake kukusanya ambayo ni bilioni 475 katika mwaka wa 2019/20 huku akibainisha kuuwa ndani ya miezi 5 tu teyari wizara yake imeshakusanya bilioni 205.
  • Ameyasema hayo leo tarehe 7/12/2019 Wilayani Nzega alikokwenda kukabidhi Leseni 11 kwa vikundi 10 vya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu. Ameongeza kuwa kuongea ongea hakusaidii zaidi ya kufanya kazi na ukifanya kazi acha namba zikusaidie kueleza unachokifanya.
1-01
Waziri wa Madini Doto Biteko akikabidhi Leseni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu kwa mmoja wa mwakilishi wa moja kati ya vikundi 10 vilivyo kabidhiwa leseni
  • Pamoja na kukabidhi leseni hizo, Biteko ametoa masherti kwenye eneo moja la uchimbaji aliloliwekea mashaka kuhusu usalama wake kutokana na hali yake huku akiagiza kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya chini ya mwenyekiti wake ambae pia ni Mkuu wa Wilaya Godfrey Ngupula  kuhakikisha utaratibu wa usalama umezingatiwa kabla ya kuanza kuchimba.
  • Vikundi vilivyokabidhiwa leseni hizo ni pamoja na; Msilale Miners Group, Jimbo la Nzega Vijijini, Undomo Miners Group, Hapa Kwetu Group, Umoja wa Wachimbaji Mwanshina, Mkombozi Mining Group, Imalamakoye Miners Group, Salama Miners, Makalanga Minerals Group na Nzega Miners Association.
  • Biteko amesema uthubutu wake na viongozi wenzake wa wizara nzima ndio unaopelekea kuiweka sekta ya madini kwenye mwendo “mdundo” huku akiahidi yeyote anayetaka kurudisha nyuma mwendo huo hatokubaliana nae.
2-01
2. Waziri wa Madini Doto Biteko akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula muda mfupi kabla ya kukabidhi leseni za kwa vikundi 10 vya wachimbaji wadogo Nzega wa kwanza kulia ni Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa
  • Ameongeza kuwa, mara kwa mara halali usiku kwa ajili ya kupokea simu za wananchi wakimpa taarifa za utoroshaji wa madini na taarifa mbalimbali. Hata hivyo amesema anakerwa na vitendo vya uchonganishi kwa kutoa taarifa za uongo huku akiwaomba wananchi kutoa taarifaa zenye ukweli na usahihi ili kulisaidia tafia.
  • “Madini haya si yangu mimi wala ya Rais John Pombe Magufuli, ni madini ya Watanzania na sote tunawajibu wa kuyalinda, kazi yangu ni kusimamia maekezo ninayopewa na Mhe. Rais na kuhakikisha sekta hii inachangia kwenye pato la taifa kama inavyostahili. Narudia tena, anae stahili sifa katika haya yote yanayofanyika kwenye madini sio Mimi Doto Biteko, anaye stahili sifa na pongezi zote ni Rais John Pombe Magufuli kwani yeye ndiye anaye elekeza na mimi ni msimamizi tuu wa kutekeleza yale anayo yaagiza.”. Alisema Biteko.
3-01
Mkurugenzi wa Leseni kutoka Tume ya Madini Mhandisi Yahaya Semamba akiwaeleza wachimbaji waliopatiwa leseni kuhusu masherti ya leseni walizopewa.
  • Kwa upande wake Mkurugenzi wa Leseni kutoka Tume ya Madini Mhandisi Yahaya Semamba amewaambia wanavikundi waliopatiwa leseni kuwa pamoja na kupatiwa leseni hizo wanapaswa kuzingati masherti ya leseni hizo na kwamba watakao kiuka watawafutia leseni yao. Miongoni mwa masherti hayo ni kuhakikisha ulipaji wa maduhuli ya serikali, kutunza mazingira, kuzingatia usalama na masherti mengine yote.
  • Akiongea kwa niaba ya wanavikundi wenzake waliokabidhiwa leseni Aluna Mgalula amemshukuru Waziri wa Madini na Mkuu wa Wilaya kwa kuwaondelea kero yao ya kupatiwa leseni. Ametoa ushuhuda wa namna alivyokuwa anamsumbua waziri Biteko kwa kumpigia simu hata usiku wa manane huku akipokea na kumsikiliza.
  • Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo wilayani Nzega ametoa pongezi kwa serikali na wizara ya madini huku akimshukuru waziri Biteko kwa namna anavyo wasaidia wachimbaji wadogo katika kuwapatia maeneo mbalimbali na kuwafanya wachimbaji kuwa na utulivu katika kazi zao.Issa Mtuwa – “WM” Nzega
Ad

Unaweza kuangalia pia

UCHUMI WA TANZANIA WAZIDI KUKUA NA KUIMARIKA

Hali ya uchumi wa Tanzania yazidi kuimarika na kukua  kwa asilimia 6.9 ikiwa ni  takwimu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *