Maktaba ya Kila Siku: January 9, 2020

NAIBU WAZIRI NDITIYE AELEKEZA SHIRIKA LA POSTA KUFANYA KAZI KIDIJITALI

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye amelielekeza Shirika la Posta Tanzania (TPC) kufanya kazi kidijitali kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhandisi …

Soma zaidi »

BANDARI YA DAR ES SALAAM YAPOKEA MELI KUBWA YA UTALII ILIYOBEBA WATALII 600

Malengo ya Tanzania kufikisha Watalii Milioni mbili kwa mwaka yameanza kutimia, baada ya Watalii  zaidi ya 600 kutoka mataifa mbalimbali duniani kuwasili nchini kwa ajili ya ya kufanya utalii katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam na Bagamoyo Mkoani Pwani. Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi (Januari 9, …

Soma zaidi »

BODI YA USHAURI YA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO (MAB) KWA TMDA, YATEMBELEA OFISI YA TMDA KANDA YA ZIWA

Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(MAB) imefanya ziara maalum na kujionea mambo mbalimbali ya utendaji kazi katika ofisi ya Kanda ya Ziwa ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA). Katika ziara hiyo, Bodi hiyo imeweza kujionea utendaji kazi za udhibiti wa …

Soma zaidi »

RAIS WA ZANZIBAR DK ALI MOHAMED SHEIN ATUNUKU NISHANI IKULU ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ametunuku Nishani ya Mapinduzi, Nishani ya Utumishi Uliotukuka pamoja na Nishani ya Ushujaa kwa Viongozi, Watumishi wa Umma, Maafisa na Wapiganaji wa Idara Maalum za SMZ na wananchi mbali mbali wenye sifa maalum. Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja …

Soma zaidi »

WAZIRI MHAGAMA ARIDHISHWA NA HATUA ZA UJENZI WA JENGO LA NEC DODOMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ametembelea na kukagua hatua ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi zilizopo eneo la Njedenwa Jijini Dodoma na kusema ameridhishwa na hatua …

Soma zaidi »

RAIS DKT. MAGUFULI AWASILI JIJINI DAR ES SALAAM AKITOKEA MAPUMZIKONI CHATO MKOANI GEITA

Rais Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 09 Januari, 2020 amewasili Jijini Dar es Salaam akitokea nyumbani kwake Chato, Mkoani Geita. Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli kesho ataanza ziara ya kikazi Visiwani Zanzibar ambako ataweka jiwe la msingi la jengo la Idara ya Usalama wa Taifa Zanzibar. …

Soma zaidi »