UMEME WA SGR KUKAMILIKA MWISHONI MWA MEI, 2020

Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa nguzo kubwa za kusafirisha umeme utakaotumika katika reli ya kisasa(SGR) kuendesha treni ya umeme, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani alifanya ziara ya kukagua njia ya kusafirisha umeme Mei 11, 2020 mkoani Morogoro.

Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa nguzo kubwa za kusafirisha umeme utakaotumika katika reli ya kisasa(SGR) kuendesha treni ya umeme, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani alifanya ziara ya kukagua njia ya kusafirisha umeme Mei 11, 2020 mkoani Morogoro.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme utakaotumika katika Reli ya kisasa ya kuendesha Treni inayotumia umeme umekamilika kwa zaidi ya asilimia 94 na utakamilika mwishoni mwa mwezi Mei 2020.

Dkt. Kalemani alisema hayo mkoani Morogoro , alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya njia ya kusafirisha umeme mkubwa, na kusema kuwa ameridhishwa na kasi ya ujenzi huo ambao unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu pamoja na kutembelea Kiwanda cha Sukari Mtibwa kuona hali ya upatikanaji wa umeme.

Ad

Alisema Kukamilika kwa mradi huo kutachangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa nchi kwa kuongeza mapato kwa kuwa umeme mwingi utakuwa ukinunuliwa kutoka Shirika la Umeme nchini (TANESCO), vilevile Shirika la Reli nchini( TRL) litapunguza gharama za kununua mafuta ya kuendesha treni.

Njia hiyo ya umeme itapita katika vituo vinne vya njia ya treni ya kisasa ambavyo ni Pugu mkoani Dar es salaam, Ruvu mkoani Pwani, Kidugaro na Kingulwira mkoani Morogoro.

“Mradi huu utakamilika ndani ya muda uliopangwa, kwa sababu tayari nguzo kubwa za umeme 450 kati ya 455 zinazotumika katika ujenzi wa njia hiyo, zimekwisha jengwa na kusalia nguzo tano(5) tu ambazo zinaendelea kujengwa ili kukamilisha ujenzi, hivyo kabla ya mwisho wa mwezi huu, mkandarasi atakuwa amemaliza kazi yote, na kitakachofuata ni kusubiri kukamilika kwa reli yenyewe ili tuanze kufanya majaribio ya umeme huo”, alisema Dkt.Kalemani.

Alisema kuwa mradi huo ni wa kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki,ukifuatiwa na Kenya ambayo imepanga kuanza kuujenga mwakani 2021,na Uganda ambayo imepanga kuanza kujenga mwaka 2025.

Mradi huo umegharimu zaidi ya shilingi za kitanzania Bilioni 72.6, na mkandarasi amekuwa akilipwa fedha zake kwa wakati.

Ad

Unaweza kuangalia pia

“KIPINDI CHA UCHAGUZI TUKIFANYA KAZI ZETU VIZURI NI KIPINDI CHA KUWAELEKEZA WATU”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *