NAIBU WAZIRI NYONGO AWATAKA VIONGOZI WA VIJIJI KUSHIRIKI KUTOA ELIMU YA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MADINI KUPUNGUZA MIGOGORO

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ameutaka uongozi wa Kijiji cha Buhunda maarufu kama Lushokela kilichocho wilayani Misungwi mkoani Mwanza kutoa elimu ya uwekezaji kwa wananchi wake ili kuwa na uelewa juu ya masuala ya uwekezaji katika sekta ya madini.

Naibu Waziri Nyongo alitoa maelekezo hayo Aprili 12, 2020 alipotembelea mradi mpya wa uchimbaji wa madini unaomilikiwa na Kampuni ya Busolwa Mining LTD uliopo katika Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, baada ya kuelezwa ugumu wa mwananchi katika kupisha mradi kwa mwekezaji huyo na kudai naye anataka kuchimba
katika eneo hilo.

Ad

“Hapa ni suala la uelewa tu, elimu ya uwekezaji katika sekta ya madini inatakiwa kwa wananchi, na watoaji wa elimu wa kwanza ni ninyi viongozi wa Serikali za vijiji na mitaa.

“Mchimbaji akiomba na kupewa leseni mmiliki wa ardhi anapaswa kulipwa fidia na kupisha eneo hilo ili kupisha shughuli za uchimbaji,”Nyongo alisisitiza.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Busolwa Mining LTD, Baraka Ezekiel akielezea jambo kwa ujumbe ulioambatana na Naibu Waziri Nyongo wakati wa ziara ya kukagua kusikiliza na kutatua changamoto za mwekezaji huyo. (Picha na Wizara ya Madini).

Kufuatia changamoto ya utoaji wa mizigo bandarini, Naibu Waziri Nyongo ameahidi kufanya mazungumzo na uongozi wa Shirika la Taifa la Usafirishaji (TASAC) kuhakikisha inaharakisha taratibu za  utoaji wa mizigo bandarini ili vifaa hivyo vitolewe kwa wakati kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo na kuwafanya wawekezaji kukamilisha miradi yao kama walivyokusudia.

Kutokana na changamoto ya ugonjwa wa Corona unaoikabili Dunia, uliopelekea baadhi ya vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya ukamilishaji wa ufungaji wa mitambo mgodini hapo kutokupatikana kwa wakati, Naibu Waziri Nyongo alisema, changamoto hiyo inaelekea ukingoni kwani nchi ya China ambako ndiko vilikiagizwa vifaa hivyo tayari viwanda mbalimbali vimefunguliwa na vinazalisha hivyo watarajie ukomo wa changamoto hiyo ndani ya muda mfupi.

Kwa upande wake Mkurugenzi na mwekezaji wa migodi ya Busolwa Mining, Baraka Ezekiel alisema wameshakusanya mchanga wa dhahabu utakaoweza kuchenjuliwa katika mgodi wao mpya wa Misungwi kwa muda wa mwaka mmoja na kubainisha kuwa, kwa sasa wanasubiri kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo uliokwamishwa kwa kiasi kikubwa na mlipuko wa janga la corona duniani.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Busolwa Mining LTD, Baraka Ezekiel akielezea jambo kwa ujumbe ulioambatana na Naibu Waziri Nyongo wakati wa ziara ya kukagua kusikiliza na kutatua changamoto za mwekezaji huyo. (Picha na Wizara ya Madini).

Akifafanua suala hilo, Baraka alisema, baadhi ya vipuri vya kukamilisha ufungaji wa mitambo katika mgodi huo ulisimama kutokana na uzalishaji wa vipuri, hivyo nchini China kusimama, lakini pia wataalamu waliokuwa wakisaidia ufungaji wa mitambo hiyo hawakuweza kurudi mara baada ya kusherehekea sikukuu za mwaka mpya wa Kichina kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa corona uliopelekea mipaka nchini humo kufugwa.

Pamoja na hayo ameeleza changamoto nyingine kuwa ni pamoja na ucheleweshwaji wa kutoa mizigo bandarini, umeme mdogo kwa ajili ya kuendeshea mitambo yao, na mgogoro wa eneo baina yake na mwananchi anayedai kutaka kuchimba madini katika eneo la leseni hiyo.

Ad

Unaweza kuangalia pia

BANDARI YA DAR ES SALAAM INAPANUKA NA KUIMARIKA: HATUA MUHIMU KWA UCHUMI WA TANZANIA

Bandari ya Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha biashara na uchumi wa Tanzania, na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *