TANI 20,000 ZA SUKARI ZIMESHUSHWA MWANZA – WAZIRI BASHUNGWA

Waziri wa viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa (Mb) amewahakikishia watanzania kuwa hakutakuwa na uhaba wa sukari tena na kuwataka wananchi wasiwe na hofu juu ya sukari na kwa wauzaji kuzingazitia bei elekezi.

Mhe.Bashungwa ameyasema hayo Tarehe 14 mai 2020 alipofika katika bandari ya Mwanza kusini na kushuhudia Shehena ya Sukari tani 20,000 ikishushwa na meli kutoka Nchini Uganda iliyoagizwa na kiwanda cha kagera sugar kwa ni niaba ya Serikali

Ad


Mhe.Bashungwa baada ya kujionea sukari ya ikishushwa amempongeza Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella na uongozi mzima wa mkoa mwanza kwa kusimamia zoezi vizuri na kwa uharaka sana;

‘‘Nakupongeza Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella na uongozi mzima wa mkoa mwanza kwa kusimamia zoezi vizuri na kwa uharaka sana kwa sababu kila mwaka viwanda vyetu vya ndani vinaposimisha uzalishaji kwa ajili ya ukarabati wa mitambo huwa ilaleta changamoto lakini  amemshukuru Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa kutambua hilo na kuona  ni kipindi  ambacho ndugu zetu Waislamu wapo kwenye mfungo wa Mwezi mtukufu wa ramadhani na kipindi hiki ambacho nchi na dunia inapambana na janga la Corona kuhakikisha upatikanaji wa Sukari kila mahali nchini na kwa kuzingatia bei elekezi’’ amesema Bashungwa

Aidha, Waziri Bashungwa amewatoa hofu watanzania kwa kuwahakikishia kuwa tatizo la sukari lilikuwepo limeisha kuanzia kwa sababu sukari ya kutosha imeshaagizwa na tayari imefika nchi na inaendelea kusambazwa kwenye mikoa mbalimbali ‘‘Watanzania wote nawaomba muendelee na mwezi mtukufu wa ramadhani vizuri Serikali tunahangaika ili kuhakikisha sukari inapatikana mikoa yote na kupanda kwa bei hakutakuwepo na niendelea kutoa wito kwa wakuu wa mikoa na Wilaya kuendelea kusimamia ukomo wa bei ambao ulitolewa na Serikali na kuhakikisha kila mtanzania anapata sukari bila bugudha yoyote ile,”alisema Mhe.Bashungwa.

Ameendelea kusisitiza kuwa ‘‘sasa hivi tumejionea Tani 20,000 zikishushwa hapa Mwanza pia na Dar es salaam tunaendelea kushusha sukari maana tuliitoa vibari vya Tani 40,000 na kampuni zilizopewa hivyo vibari mpaka sasa kampuni hizo zinaendelea kushusha sukari”

Ad

Unaweza kuangalia pia

Je! Wajua Mchango wa Madini ya Tanzanite katika Pato la Taifa?

Madini ya Tanzanite, yanayopatikana pekee katika eneo dogo la Mererani, Tanzania, ni miongoni mwa rasilimali …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *