WIZARA YA ARDHI YAPOKEA VIFAA VYA ZOEZI LA URASIMISHAJI MAKAZI

Wizara wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi imepokea  vifaa kwa ajili ya uanzishaji wa masjala za kutunza nakala za hati za umiliki wa ardhi ikiwa sehemu ya zoezi la urasimishaji wa makazi linalofanyika nchi nzima.

Vifaa vilivyotolewa wa kompyuta tano (5) na mashine mbili (2) za uchapishaji wa nyaraka mbalimbali za urasimishaji wa makazi.

Ad

Akizungumza wakati wa tafrija fupi ya kukabidhi wa vifaa hivyo iliyofanyika katika ofisi za Ardhi jijini Dar es salaam, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi alisema kuwa uanzishwaji wa masjala hizo ni sehemu ya utakelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli aliyeagiza Wizara ya Ardhi kuondoa kero zote za ardhi zinazowakabili wananchi.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akihimiza jambo wakati wa tafrija fupi ya kukabidhi kwa vifaa kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za Wizara ya Ardhi za kuanzisha masjala za kutunza nakala za hati za umiliki wa ardhi ikiwa sehemu ya zoezi la urasimishaji wa makazi linalofanyika nchi nzima.

“Niwashukuru Benki ya Maendeleo ya TIB ya kuunga jitihada hizi za kuweza katika kuanzisha masjala hizi ambazo ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Rais, hivyo zitasaidia kupunguza kero za Watanzania wanaposhughulikia masuala ya umiliki wa ardhi.” alisema.

Waziri Lukuvi alisema kuwa lengo la urasimishaji ni kuhakikisha usalama wa milki na kuwezesha upatikanaji wa maeneo kwa ajili huduma za kijamii na miundombinu kwa njia shirikishi.

Aliongeza kuwa zoezi hili litasaidia mzunguko wa fedha na kuimarisha uchumi kwa kuwa utasaidia wananchi kutumia nyumba zao kama dhamana ili kuweza kukopa katika taasisi za kifedha pia, litasaidia kuzipa fursa taasisi hizo kuweza kuhakiki umiliki wa waombaji wa mikopo.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi (kulia) akipokea kompyuta zilizotolewa na Benki ya Maendeleo TIB kuunga mkono uanzishaji wa masjala za kutunza nakala za hati za umiliki wa ardhi ikiwa sehemu ya zoezi la urasimishaji wa makazi linalofanyika nchi nzima. Anayekabidhi kompyuta hizo ni Mkurugenzi wa Mipango, Mikakati na Mahusiano wa Kitaasisi za Benki ya Maendeleo ya TIB, Bw. Patrick Mongella (kushoto)

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mipango, Mikakati na Mahusiano wa Kitaasisi za Benki ya Maendeleo ya TIB, Bw. Patrick Mongella alisema kwa kiasi kikubwa taasisi za kifedha zinaitegemea Wizara ya Ardhi kwa ajili ya utoaji wa mikopo kwa watu na taasisi mbalimbali ambao wanatumia ardhi kama sehemu ya dhamana ya mikopo yao.

“Zoezi hili ni muhimu kwa taasisi za fedha ikiwemo TIB kwa kuwa kwa kiasi kikubwa shughuli za ukopeshaji zinatumia ardhi kama sehemu ya dhamana ya mikopo,” alisema.

Bw. Mongella aliongeza kuwa TIB kama benki ya Serikali iliona ni fursa nzuri ya kuunga mkono jitihada za wizara hili kuisaidia katika uwekaji wa kumbukumbu katika zoezi la urasimishaji wa ardhi.

Zoezi la urasimishaji wa makazi linahusisha kutambua, kupanga, kupima na kumilikisha maeneo yaliyoendelezwa bila kupangwa. Akiwasilisha Bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ardhi kwa Mwaka wa fedha 2020/2021 hivi karibuni, Waziri Lukuvi alisema katika kipindi cha miaka mitano Wizara ya Ardhi imeweza kuidhinisha michoro ya Mipangomiji ya urasimishaji yenye viwanja 703,836.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *