WAZIRI MKUCHIKA AZINDUA BODI YA USHAURI YA WAKALA YA NDEGE ZA SERIKALI

James K. Mwanamyoto – Chamwino DodomaSerikali imezindua Bodi ya Ushauri ya Wakala ya Ndege za Serikali ambayo itakuwa na jukumu la kumshauri Waziri mwenye dhamana juu ya namna bora ya kuboresha wakala hiyo ili kuwa na mipango na mikakati endelevu itakayoleta tija katika usafiri wa anga.


Akizindua bodi hiyo mapema leo Ikulu ya Chamwino, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) ameitaka bodi kuhakikisha Tanzania inakuwa na Shirika la Ndege imara litakaloweza kushindana na mashirika mengine ya kikanda na kimataifa kwa kuanzisha na kuendesha safari nyingi za ndani ya nchi, za kikanda na za kimataifa.

Ad
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakala ya Ndege za Serikali (hawapo pichani) mara baada ya kuzindua Bodi hiyo mapema leo Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.


Mhe. Mkuchika amesema, suala la kuimarisha usafiri wa anga kwa kulifufua Shirika la Ndege la Tanzania ni moja ya utekelezaji wa ahadi za Chama cha Mapinduzi iliyopo kwenye ilani yake ya Uchaguzi ya Mwaka 2015. Mhe. Mkuchika ameitaka Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) na Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kufanya kazi kwa ushirikiano wenye tija ikiwa ni pamoja na kujengeana uwezo na uzoefu kiutendaji.


Aidha, Mhe. Mkuchika amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kulipa uzito mkubwa jukumu la usimamizi wa TGFA kwa kumteua Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. BaloziMhandisi John W. H. Kijazi kuwa Mwenyekiti ya Bodi ya Ushauri wa Wakala ya Ndege za Serikali.


Kwa upande wake, Mhe. Balozi Mhandisi John W. H. Kijazi, amemshukuru Mhe. Rais kwa kumuamini na kumpa jukumu la kuongoza bodi hiyo ili iweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Mhandisi John W. H. Kijazi ambaye pia ni Mwenyekiti ya Bodi ya Ushauri wa Wakala ya Ndege za Serikali akitoa neno la shukrani mara baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) kuzindua rasmi bodi hiyo mapema leo Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.


Mhe. Balozi Kijazi ameahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri Mkuchika ili kuiwezesha Wakala ya Ndege za Serikali kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kuliimarisha Shirika la Ndege ya Tanzania kuwa imara na la kiushidani.


Wakala ya Ndege za Serikali ilianzishwa rasmi tarehe 17 Mei, 2002 kupitia Sheria ya Wakala za Serikali Na. 30 ya Mwaka 1997 kama ilivyorekebishwa Mwaka 2009. Wakala hii, ilikuwa chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi naMawasiliano ambapo tarehe 23 Aprili, 2018, Serikali iliamuia kuihamishia Ofisi ya Rais, Ikulu kwa Tangazo la Serikali Na. 252 la tarehe 8 Juni, 2018.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Benki ya NMB Tanzania yapongezwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

kwakuwa Kinara katika utendaji wake, kutengeneza faida kubwa ya mfano wa kuigwa na mashirika na …

2 Maoni

 1. Теневой плинтус: стильное решение для обновления интерьера,
  Как правильно установить теневой плинтус своими руками,
  Как использовать теневой плинтус для создания уникального интерьера,
  Ретро-стиль с использованием теневых плинтусов: идеи для вдохновения,
  Советы стилиста: как сделать цвет теневого плинтуса акцентом в помещении,
  Теневой плинтус: простое решение для скрытия кабелей и проводов,
  Интересные решения с теневым плинтусом и подсветкой: идеи для вдохновения,
  Современные тренды в использовании теневого плинтуса для уюта и красоты,
  Интерьер безупречный до мелочей: роль теневого плинтуса в декоре
  купить плинтус https://plintus-tenevoj-aljuminievyj-msk.ru/ .

 2. безопасно,
  Индивидуальный подход к каждому пациенту, для поддержания здоровья рта,
  Профессиональное лечение и консультации, для вашей улыбки,
  Индивидуальный подход к каждому пациенту, для вашего здоровья и благополучия,
  Эффективное лечение зубов и десен, для вашего долгосрочного удовлетворения,
  Профессиональная гигиена полости рта, для вашего комфорта и удовлетворения,
  Индивидуальный план лечения для каждого пациента, для вашего здоровья и благополучия
  дитяча стоматологічна https://stomatologichnaklinikafghy.ivano-frankivsk.ua/ .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *