DKT KALEMANI AAGIZA WANANCHI WAUNGANISHIWE UMEME NDANI SIKU 21

Hafsa Omar-Dar es Salaam

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ametoa agizo kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini( REA) pamoja na wakandarasi wote kuhakikisha kuwa wananchi wote waliolipia huduma ya umeme waunganishiwe  umeme ndani ya siku 21.

Ad

Alitoa agizo hilo Oktoba 5,2020 wakati akiwa kwenye ufunguzi wa kiwanda cha kuzalisha mita luku cha Multicable Ltd kilichopo katika Wilaya ya Temeke,jijini Dar es Salaam.

Aidha, alisema wananchi takribani 5000 nchini wamelipia huduma hiyo na hadi sasa hawajaunganishiwa  na huduma hiyo ambayo ni muhimu katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na kwa nchi kiujumla.

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani(mwenye miwani)akietembelea kwenye maeneo mbalimbali ya kiwanda cha kuzalisha mita za luku cha Multicable ltd, kilichopo katika Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam,akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa Taasisi za Wizara na Nishati, na wameliki wa kiwanda cha Multicable ltd,Oktoba 5,2020.

Dkt.Kalemani, ameleeza kuwa uwepo wa viwanda vingi vya ndani ambavyo vinazalisha vifaa vya usambazaji wa umeme kunarahisha usambazaji wa umeme nchini  na hakuna tena sababu yoyote ambayo itapelekea ucheleweshaji wa  uunganishaji umeme kwa wananchi.

“ nimeshaeleza hapo mwanzo kuwa  hakuna tena sababu zinazosababisha  wananchi wachelewe  kupata umeme  kwa kisingizio cha uhaba wa mita za luku, kwenye kiwanda hiki ambacho nimekifungua leo kuna takribani mita za luku 500,000 ambazo zipo tu hata hazijanunuliwa”alisema Dkt.Kalemani.

Pia, amewataka wakandarasi wanaotekeleza mradi wa REA kukamilisha kazi zao ifikapo tarehe 15 Oktoba mwaka huu, kwakuwa vifaa vyote vinavyohitaji kwaajili ya usambazaji umeme vinapatikana kwenye viwanda nchini,ambavyo ni vya bei rahisi na vyenye ubora wa viwango vya juu.

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani(mwenye miwani)akietembelea kwenye maeneo mbalimbali ya kiwanda cha kuzalisha mita za luku cha Multicable ltd, kilichopo katika Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam,akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa Taasisi za Wizara na Nishati, na wameliki wa kiwanda cha Multicable ltd,Oktoba 5,2020.

“wakandarasi wote ambao miradi yao imekaribia kukamilika ambao wengi wao amebakiza vijiji 2 au 3, wakamilishe kazi zao kwa haraka na hatutawaongezea muda na ifikapo Oktoba 15 mwaka huu wakabidhi miradi yao”alisema.

Aidha, amewataka wananchi wote ambao hawajafikiwa na huduma ya umeme kwenye maeneo yao nchini watulie, na kuamini Serikali yao, kwani  tayari Serikali imeshatekeleza miradi mingi na mpango wa Serikali ni kuhakikisha kuwa umeme unafika kwa wananchi wote ambao hawajafikishiwa umeme ndani ya miaka miwili ijayo.

Alieleza kuwa, Serikali imejipanga vizuri kuhakikisha huduma ya umeme inapatikana nchini kote na kuwataka wawekezaji nchini kuendelea kufungua viwanda vingi zaidi vya vifaa vya usambazaji wa umeme,ambapo ameeleza kuwa kufunguliwa kwa viwanda vingi  kutawarahisishia wananchi kupata umeme kwa muda mfupi zaidi.

Amesema, Serikali itahakikisha inavilinda viwanda  vyote vya kuzalisha mita za luku nchini ambavyo mpaka sasa vimefunguliwa viwanda takribani  10 vya uzalishaji huo, ambavyo  vinasaidia kutaoa ajira nyingi kwa watanzania na Serikali imejipanga kuhakikisha inavilinda viwanda hivyo kwa kuwatafutia  soko la kuzia bidhaa zao.

Pia, amewashukuru wawekezaji wa viwanda vya kutengenezea vifaa vya kusambazaji umeme nchini,viwanda hivyo ambavyo vimesaidia sana kutatua changamoto ya upatikanaji wa vitendea kazi vya usambazaji umeme nchini.

Vilevile, amewahamasisha wawekezaji mbalimbali  nchini kuendelea kuwekeza katika viwanda vya kuzalisha mita za kusambazia gesi majumbani.

Ambapo ameeleza kuwa, tayari Serikali imeshaweka zuio kwamba ifikapo januari wakandarasi wote watakaopewa kazi ya usambazaji gesi majumbani hawataruhusiwa kuagiza mita kutoka nje ya nchi ili kulinda soko la ndani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kiwanda cha Multicable ltd , Murtaza Alibhai amesema kuwa wameamua kutekeleza sera ya Rais wa awamu ya tano, ya Tanzania ya  viwanda kwa vitendo ili kuendana na kasi ya ukuaji wa uchumi nchini, ambapo amesema kiwanda hicho mpaka sasa kimeajiri zaidi ya wafanyakazi 700.

Amesema kiwanda chao kitahakikisha kuwa kinazalisha bidhaa bora zenye viwango vya hali ya juu ili kuchangia uchumi kupitia sekta ya  viwanda.

Aidha, ameeleza kuwa kampuni hayo inatarajia kuanzisha kiwanda cha kutengeneza transifoma hivi karibuni ili kuhakikisha kuwa usambazaji umeme nchini unafanyika kwa haraka na watanzani wote wafurahiye kupata huduma ya umeme.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Uzinduzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya UCSAF Dodoma: Kuimarisha Mawasiliano Vijijini

25 Aprili 2024, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *