








Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Malawi Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera wameweka jiwe la msingi la ujenzi wa stendi Kuu ya Mabasi yaendayo Mikoani na nchi jirani , eneo la Mbezi mwisho Jijini Dar es Salaam leo tarehe 08 Oktoba 2020.
Akizungumza katika hafla hiyo Rais Magufuli amesema kuwa stendi hiyo iwekwe ofisi ya Uhamiaji kwani stendi hiyo ni ya kimataifa na kuongeza kuwa katika kupangwa kwa eneo hilo kuwekwe eneo la mabasi yanayotoka nje ya nchi ili kurahisisha kutoa huduma.
“Mabasi yanatoka nje ya nchi yawe na sehemu yao ya maengesho, mabasi ya humu yawe na sehemu yao, daladala yawe na sehemu yao, bajaji ziwe na sehemu yao, mama lishe wawe na sehemu zao, hapo pataweza kuleta umaana wa stendi hii na hapo unaweza ukaleta umaana wa fedha za walipa kodi ambao ambao ni watanzania wote” amesema Rais Magufuli
Aidha, Rais Magufuli amesema kuwa amefurshishwa kushuhudia mradi huo kwani mradi huo ni “MATOKEO CHANYA ya miradi inayofanywa na Serikali.