SERIKALI YA TANZANIA YATIA SAINI MKATABA WA HGA NA WAWEKEZAJI WA MRADI WA EACOP.

Na.Vero Ignatus Arusha.

Majadiliano ya kutia saini mkataba wa nchi hodhi baina ya Total na Serikali ya Tanzania juu ya utekelezaji wa mradi wa EACOP umefanyika leo Jijini Arusha katika hotel ya Grad melia.

Ad

 Utiaji wa saini wa makubaliano ya awali ya Afrrika ya mashariki (EACOP )kati ya serikali ya Tanzania katika makubaliano ya serikali mwenyeji (HGA)  ambapo mradi huo utafungua fursa Afrika ya Mashariki kwa kuvutia wawekezaji 

Akizungumza na waandishi wa habari mwanasheria Mkuu wa Serikali Prof. Adelardus Kilangi, katika hafla ya utiaji saini Jijini  Arusha, alisema kuwa mradi huo utapelekea kuongezeka kwa fedha za kigeni zaidi ya 60% ,ya fedha za moja kwa moja za kigeni (FDI), Uganda na Tanzania katika kipindi cha ujenzi,ambapo msingi wa mafanikiao wa mradi huom utapatikana kupitia ushirikiano mzuri na uelewano wa wadau wote

Alisema kusainiwa kwa makubaliano ya masuala ya pamoja kati ya Rais wa Tanzania Dkt.John Magufuli, na Rais Yoweri Museven wa Uganda, ambapo ni makubaliano katika mradi baina ya nchi mbili, walikubaliana kwamba kila nchi kwa uharaka itakamilisha makubaliano ya serikali mwenyeji kwa upande wa mradi

Alisema kuwa hatua hiyo ya msingi wa utekelezaji wa mradi wa EAPOC, ni kielelezo cha mafanikiao mengine katika mchakato wa kufuatia makubaliano ya awali ,ya serikali mwenyeji upande wa Uganda mnamo tarehe 11septemba 2020.

Prof.Kilangi alitoa wito kwa wawekezaji wengine wote waje wanakaribishwa na wasitiwe hofu na mtu yeyote,wanakaribishwa Tanzania mazingira ni mazuri na majadiliano yanafanyika katika hali njema ya uwazi ,kuhakikisha kuwa mwekezaji anapoata na Taifa linapata pia

Prof.Kilangi alisema kuwa bomba hilo la mafuta Ghafi Afrika ya mashariki linaundwa na bomba la inchi 24 linalotunza joto na kufunika ardhi,vituo sita vya kusukuma mafuta,(viwili vikiwa nchini Uganda na vinne nchini Tanzania)viwili vya kupunguza kasi ya mafuta na vyote vipo nchini, ambapo mafuta ya uganda yapo katika hali ya joto na yanahitaji kusafirishwa katika kiwango cha nyuzi joto 50c ili yaweze kufikia kiwango ncha kutiririka

Kwa upande wake Rais wa Utafutaji na Uzalishaji Total, Afrika Nicolas Terraz alisema kuwa amefurahishwa na majadiliano yaliyoonzwa na msaidizi wake Martin Tiffed na kusema yale yote yaliyosemwa watayatilia maanani na kuyaingiza katika utendaji 

Aidha alisema kuwa katika mradi huo vifaa mbalimbali vitakavyonunuliwa vitagharimu jumla ya shilingi za kitanzania trilion 1.7 ambapo kutakuwa na fursa ya usafirishaji wa mizigo ,makadirio yake yatakuwa shilingi bil 496,Ajira 10,000 malipo yake au misahara itakuwa shilingi za kitanzania  bilion 294,kutakuwa na fursa mahusussi kwaajili ya watanzania .

Ad

Unaweza kuangalia pia

“Nani aliyeunda Jumuiya ya Madola na kwa nini?”

Malkia Elizabeth II pamoja na mawaziri wake wakuu wa Jumuiya ya Madola mwaka 1962. Picha: …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.