RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Adelardus Lubango Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja wa Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 09 Novemba 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 09 Novemba, 2020 amemuapisha Prof. Adelardus Lubango Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Lubango Kilangi alipokuwa akila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja wa Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali katika Ikulu ya Chamwino mara baada ya kumuapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Lubango Kilangi leo tarehe 09 Novemba 2020.

Hafla ya kuapishwa kwake imefanyika Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Ibrahim Hamis Juma, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na viongozi wengine mbalimbali.

Ad
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali katika Ikulu ya Chamwino mara baada ya kumuapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Lubango Kilangi leo tarehe 09 Novemba 2020.

Akizungumza baada ya kumuapisha Mhe. Rais Magufuli amesema Watanzania wana matumaini makubwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wanataka kuona Serikali yao inapata uwakilishi mzuri katika masuala ya kisheria, hivyo amemtaka kuhakikisha anasimamia vizuri kesi za Serikali na kuzitetea kwa uharaka mali za Serikali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Lubango Kilangi muda mfupi baada ya kumuapisha leo tarehe 09 Novemba 2020 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

“Watanzania hawapendi kuona Serikali yao inashindwa katika kesi, kachape kazi, kawatetee Watanzania hasa wanyonge, katetee mali za Serikali na kwa haraka. Umefanya kazi nzuri katika kipindi chako cha kwanza, nataka ukafanye kazi vizuri zaidi, ukajipange sawasawa, ndio maana nakupongeza lakini wakati huo huo nakupa pole kwa majukumu haya” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amewatoa hofu viongozi wateule wote ambao wamekuwa na hofu ya kuondolewa ama kubadilishwa katika nafasi walizonazo baada ya yeye kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha pili, akisema hatarajii kufanya mabadiliko ya viongozi hao labda kwa wale watakaokuwa wanastaafu ama kutofanya vizuri katika majukumu yao.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka mara baada ya hafla fupi ya Uapisho katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 09 Novemba 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka mara baada ya hafla fupi ya Uapisho katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 09 Novemba 2020. PICHA NA IKULU
 

“Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Wilaya, Wakurugenzi, Viongozi wa Taasisi na Idara za Serikali na wengine wote chapeni kazi, simuondoi mtu kwenye nafasi yake labda aharibu yeye mwenyewe au astaafu” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Msalaba Mwekundu: Nguzo ya Kibinadamu na Ujenzi wa Jamii Imara

Msalaba Mwekundu, ambao ni sehemu ya Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *