WAKUU WA MIKOA,WAKUU WA WILAYA MSIWE NA WASIWASI CHAPENI KAZI – RAIS MAGUFULI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amewatoa hofu Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwani ameanza nao na atamaliza nao.

Rais Magufuli amesema hayo katika hafla ya kumwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Prof. Adelardus Kilangi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Chamwino jijini Dodoma.

Ad

“Mkuu wa mkoa unakuwa na wasiwasi gani labda kama ulikuwa ufanyi kazi vizuri kwasababu nashangaa napata vimesji vingine Mhe Rais nimejitahidi katika kipindi changu kana kwamba kipindi chake nilimwambia kinaisha baada ya mimi kuapishwa nimeona hili nilizungumze kwamba Wakuu wa Mikoa,Wakuu wa Wilaya msiwe na wasiwasi” Amesema Rais Magufuli

Rais Magufuli amesema kuwa kunaweza kusitokee mabadiliko katika nafasi hizo isipokuwa kwa mtu anayestaafu au atakayefanya mambo ya hovyo “kwanini nibadilishe Mkuu wa mkoa, kwanini nibadilishe mkuu wa Wilaya, kwanini nibadilishe Mkurugenzi, kwanini nibadilishe DAS Serikali ni ile ile” Amesema Rais Magufuli

Rais Magufuli amewataka watendaji hao KUCHAPA KAZI kwani anajua alianza nao na atamaliza nao, ameongeza kuwa hata kwa watendaji wengine akitolea mfano Makatibu Wakuu nao itakuwa hivyo hivyo.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdory Mpango, tarehe 01 Novemba 2024 ameungana na kuongoza Waombolezaji Katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo,jijini Dar-es-Salaam, kuaga mwili wa marehemu Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali David Bugozi Musuguri

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *