Mkutano wa Ushirikiano wa Uchumi na Biashara kati ya Afrika na China umefanyika jijini Jinhua katika Jimbo la Zhejiang na kuhudhuriwa na Wanadiplomasia wa Nchi za Afrika, viongozi wa Serikali ya Jimbo la Zhejiang na Mji wa Jinhua pamoja na wafanyabiashara wa China na Afrika.
Katika mkutano huo Naibu Katibu Mkuu wa Jimbo la Zhejiang Ndugu GAO Yi ameeleza kwamba katika kipindi cha miaka 20 biashara kati ya China na Afrika imeongezeka mara 20 hadi kufikia Dola za Kimarekani Bilioni 208.7. Na uwekezaji umeongezeka mara 100 hadi kufikia USD Bilioni 49.1
Kwa upande wake Balozi Kairuki ameshauri China ifungue zaidi fursa kwa wafanyabiashara wa Afrika kuuza bidhaa katika soko la China ili kupunguza nakisi ya biashara iliyopo ambapo China ndio inauza ziadi katika soko la Afrika kuliko Nchi za Afrika zinavyouza katika soko la China.
Vilevile Balozi Kairuki ameishukuru China kwa kutoa fursa kwa makampuni ya Afrika kushiriki katika maonesho ya 3 ya Bidhaa za Nje China International Import Expo yanayoendelea jijini Shanghai ambapo bidhaa mbalimbali kutoka Afrika zimepata masoko ikiwemo Korosho, ufuta na mvinyo kutoka Tanzania