ALLAN KIJAZI AKABIDHI MAGARI 9 YA MRADI WA KUSIMAMIA MALIASILI NA KUKUZA UTALII KUSINI MWA TANZANIA

Kamishna wa Uhifadhi TANAPA na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi jijini Dodoma amekabidhi magari 9 ya Mradi wa Kusimamia Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa Hifadhi za Mikumi, Ruaha na Udzungwa.

Dkt.Kijazi amesema kuwa magari haya yatatumika kuimarisha na kuboresha shughuli za uhifadhi na utalii katika hifadhi husika.

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi Mwandamizi Betrita Lyimo anayesimamia mradi huo kwa upande wa TANAPA
amesema kuwa magari haya ni awamu ya pili ya magari 23 yaliyolengwa kwa ajili ya mradi huo na kusema kuwa magari haya yanatarajiwa kuimarisha shughuli za doria pamoja na kuhudumia watalii.

Naibu Kamishna Steria Ndaga ambaye ni Mkuu wa Kanda ya Mashariki aliahidi kusimamia magari hayo pamoja na mipango mingine yote ili kuhakikisha kuwa lengo la mradi huo kwa ukanda wa kusini linatimizwa kwa wakati na kuleta tija ilihokusudiwa.

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI MKENDA AWATAKA WADAU WA NDIZI KUCHANGAMKIA FURSA

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda (Mb) akizungumza wakati wa akifungua mkutano wa wadau …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.