DC CHONGOLO AFANYA ZIARA UKAGUZI WA MIUNDOMBINU SHULE YA MSINGI BOKO

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo ametembelea shule ya msingi Boko kwa lengo la kukagua changamoto zilizojitokeza katika miundombinu ya shule hiyo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Akizungumza na uongozi wa shule katika ziara hiyo Chongolo ameeleza kuwa eneo hilo limekuwa na changamoto ya kujaa maji nyakati za mvua na kwamba linapaswa kufanyiwa ukaratabati wa haraka ili kuepuka madhara makubwa yanayoweza kujitokeza.

Ad

Amesema “Ukiangalia hapa miundombinu ya shule siorafiki kwa watoto kutokana na changamoto hii ya kujaa maji wakati wa mvua, hapa tunaona maji yamezunguka shule, na ni mvua ya siku mbili tu iliyonyesha, sasa natoa wiki mbili, nitarud hapa tarehe 25 kuangalia nini kimefanyika, pesa zipo zifanye kazi kwa ajili ya watoto wetu wasome kwenye mazingira mazuri” Chongolo.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo akipokelewa na uongozi wa shule ya Msingi Boko alipotembelea shule hiyo kwa lengo la kukagua miundombinu ya shule hiyo baada ya mvua kunyesha.

Awali Mhandisi wa Manispaa hiyo Ndg Mkelewe Tungaraza alimueleza Mkuu wa Wilaya hatua anuai zilizokwisha chukuliwa kwa lengo la kutatua changamoto hiyo iliyodumu kwa muda mrefu hasa kipindi Cha mvua.

“Mkuu wa Wilaya , Manispaa tulishatenga kiasi cha fedha za kitanzania milioni 70, na ujenzi huu wa mifereji tutatumia mfumo wa Force Account, hadi sasa tunavyo zungumza pesa zipo tayari na kinachofanyika hivi sasa tunaongea na mkandarasi ili ujenzi huu uanze haraka iwezekanavyo” amesema Mhandisi Tungaraza.

Katika ziara hiyo, Mhe. Chongolo aliambatana na Afisa Elimu Msingi, Mchumi, Mkuu wa Idara ya Ardhi, Mipango miji na Maliasili pamoja na Afisa Mazingira wa Manispaa ya Kinondoni.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Mkutano wa Tatu wa Jukwaa la Haki za Watoto

Tarehe 4 hadi 5 Aprili 2024, umefanyika Mkutano wa Tatu wa Jukwaa la Haki za …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *