RAIS MSTAAFU DKT. KIKWETE AMEWATAKA VIJANA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUZICHANGAMKIA FURSA ZILIZOPO

Rais Mstaafu ,Dkt Jakaya Kikwete  amewataka vijana wa jumuiya ya Afrika Mashariki kuhakikisha  wanashiriki kikamilifu katika jumuiya ya Afrika mashariki na kuweza kuzichangamkia fursa zilizopo.

Aliyasema hayo jana wakati akifungua mkutano wa vijana wa jumuiya ya Afrika mashariki (YouLead)uliofanyika  mkoani Arusha.

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akipiga selfie na Vijana na wadau mbalimbali baada ya kufungua rasmi mkutano wa vijana wa jumuiya ya Afrika Mashariki (YouLead)uliofanyika mkoani Arusha jana

Kikwete alisema kuwa, ushirikiano katika Jumuiya ya Afrika mashariki ulianza muda mrefu na  ni jukumu la vijana kuhakikisha  wanashiriki kikamilifu kwani asilimia 80 ya watu walioko katika jumuiya hiyo ni vijana.

Ad
Ad

Unaweza kuangalia pia

Mkutano wa Tatu wa Jukwaa la Haki za Watoto

Tarehe 4 hadi 5 Aprili 2024, umefanyika Mkutano wa Tatu wa Jukwaa la Haki za …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *