RAIS MAGUFULI – TRA JIREKEBISHENI KWA KUTENDA HAKI KWA WAFANYABIASHARA

Rais wa. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwasili mtaa. wa Lumumba jijini Dar es salaam kuzindua rasmi jengo la Jitegemee House pamoja na Studio za Channel Ten Plus,Radio Magic FM na Radio Classic FM leo Alhamisi Februari 25, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli tarehe 25 Februari, 2021 ameendelea na ziara yake Mkoani Dar es Salaam ambapo ameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Soko Kuu la Kisutu, amezindua jengo la Jitegemee na amezindua vyombo vya habari vya kampuni ya Afrika Media Group Limited inayomiliki vituo vya luninga vya Channel Ten na Channel Ten Plus, na vituo vya redio vya Magic FM na Classic FM.

Soko Kuu la Kisutu lenye ghorofa 4 kwenda juu na 1 kwenda chini (basement) limejengwa upya likiwa na uwezo wa kuchukua wafanyabiashara zaidi ya 1,500 ikilinganishwa na soko la zamani lililokuwa na uwezo wa kuchukua wafanyabiashara 669, kuegesha magari 40, lina maeneo ya huduma za kijamii na lina eneo la ukubwa wa meta za mraba 11,935.

Ad
Rais wa. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwasili mtaa. wa Lumumba jijini Dar es salaam kuzindua rasmi jengo la Jitegemee House pamoja na Studio za Channel Ten Plus,Radio Magic FM na Radio Classic FM leo Alhamisi Februari 25, 2021

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Joseph Nyamuhanga amesema ujenzi wa soko hili ambao umefikia zaidi ya asilimia 95 utagharimu shilingi Bilioni 13.484 (fedha zote zikiwa zimetokana na makusanyo ya ndani ya iliyokuwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala) na kukamilika kwake kutawahakikishia wazalishaji wa bidhaa hasa wakulima kupata soko na kuinua kipato cha wafanyabiashara wakiwemo wafanyabiashara wadogo (Machinga) takribani 2,000.

Rais wa. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea maeneno mbalimbali baada ya kuzindua rasmi jengo la Jitegemee House pamoja na Studio za Channel Ten Plus,Radio Magic FM na Radio Classic FM leo Alhamisi Februari 25, 2021

Jengo la Jitegemee ambalo linamilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) limekarabatiwa kwa gharama ya shilingi Milioni 800 baada ya kutelekezwa kwa takribani miaka 16.

Jengo hilo la kihistoria lilijengwa mwaka 1961 na Chama cha TANU ambacho kutokana na Wakoloni kutotaka kujenga vyuo vikuu kwa ajili ya Watanzania kiliamua majengo hayo yatumike kuanzisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Rais wa. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika studio mpya za Magic FM baada ya kuzindua rasmi jengo la Jitegemee House pamoja na Studio za Channel Ten Plus,Radio Magic FM na Radio Classic FM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo Alhamisi Februari 25, 2021

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Bashiru Ally Kakurwa amesema CCM inajisikia fahari kuwa chimbuko la kupigania elimu kwa Watanzania kwa kuanzisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (kikiwa na wanafunzi 14) ambacho leo kimekua hadi kuwa shule 7, ndaki 7, Vyuo Vikuu Vishiriki 2, Taasisi 6 na wanafunzi 35,330.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akibofya kitufe kuzindua rasmi studio mpya za Channel Ten Plus TV, Radio Magic FM na Radio Classic FM katika jengo la Jitegemee mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo Alhamisi Februari 25, 2021

Baada ya kuzindua jengo hilo, Mhe. Rais Magufuli amezindua na kukagua vyombo vya habari vya kampuni ya Africa Media Group Limited inayomilikiwa na CCM ambavyo ni Channel Ten, Channel Ten Plus, Magic FM na Classic FM ambavyo pamoja na kuhamishiwa katika jengo hilo vimefungwa mitambo na vifaa vipya vya matangazo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia wimbo wa “BABA” Wasanii Profesa Jay na Stamina wakati alipozindua rasmi studio za Channel Ten Plus TV katika jengo la Jitegemee mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo Alhamisi Februari 25, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia wimbo wa “BABA” Wasanii Profesa Jay na Stamina wakati alipozindua rasmi studio za Channel Ten Plus TV katika jengo la Jitegemee mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo Alhamisi Februari 25, 2021
Rais wa. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiondoka baada ya kuzindua rasmi jengo la Jitegemee House pamoja na Studi za Channel Ten Plus,Radio Magic FM na Radio Classic FM leo Alhamisi Februari 25, 2021

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli ameipongeza iliyokuwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ambayo kutokana na kuongoza katika ukusanyaji wa mapato ya ndani hapa nchini imefanikiwa kujenga Soko Kuu la Kisutu kwa kutumia fedha zake, na amesema baada ya kuipandisha hadhi na kuwa Jiji la Dar es Salaam Meya na Naibu Meya waliokuwa wa Manispaa ya Ilala ndio watakuwa Meya na Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi wa jengo jipya la Soko Kuu la Kisutu katika Barabara ya Bibi Titi Mohamed jijini Dar es salaam

Rais Magufuli ameeleza dhamira yake ya kuhakikisha Jiji la Dar es Salaam linaboreshwa kwa miundombinu na huduma mbalimbali za kijamii na amebainisha kuwa Soko Kuu la Kisutu ni kati ya Masoko 22 yaliyojengwa katika miji mbalimbali hapa nchini kwa gharama ya shilingi Bilioni 119.921 na vituo vya mabasi 18 ambavyo vimewekewa ta ana kujengwa barabara za kuingia na kutoka.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifunua kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi wa jengo jipya la Soko Kuu la Kisutu katika Barabara ya Bibi Titi Mohamed jijini Dar es salaam

Rais Magufuli ametaka Soko Kuu la Kisutu litunzwe vizuri, amewataka wafanyabiashara kuwa waadilifu kwa kulipa kodi inavyostahili badala ya kukwepa kwa kutumia Wamachinga na ametaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kujirekebisha kwa kutenda haki kwa wafanyabiashara kwani baadhi ya maafisa wake wamekuwa wakiwatisha wafanyabiashara kwa makadirio makubwa ya kodi ili kupata mwanya wa kupokea rushwa.

Muonekano kutoka angani wa jengo jipya la Soko Kuu la Kisutu katika Barabara ya Bibi Titi Mohamed jijini Dar es salaam ambalo limekewa jiwe la msingi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli

Aidha, Rais Magufuli ameipongeza CCM kwa uwekezaji mzuri wa jengo la Jitegemee na amewapongeza wafanyakazi wa Africa Media Group Limited wakiwemo waandishi wa habari na Watangazaji ambao amewataka kufanya kazi kwa weledi na kutanguliza maslahi ya Taifa.

Muonekano kutoka angani wa jengo jipya la Soko Kuu la Kisutu katika Barabara ya Bibi Titi Mohamed jijini Dar es salaam ambalo limekewa jiwe la msingi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli

Ad

Unaweza kuangalia pia

Uzinduzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya UCSAF Dodoma: Kuimarisha Mawasiliano Vijijini

25 Aprili 2024, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *