WAZIRI LUKUVI AMALIZA UTATA MGOGORO WA ARDHI KIJITONYAMA

Na Munir Shemweta, WANMM


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amemaliza utata uliojitokeza mtaa wa Nzasa kata ya Kijitonyama katika Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam baina ya baadhi ya wakazi wa mtaa huo na mmiliki wa viwanja  namba 296 na 297 Dkt Khalifa Mussa Msami kuhusiana na umiliki pamoja na mipaka ya eneo hilo.

Ad


Waziri Lukuvi alienda katika eneo hilo lililopo barabara ya Segera tarehe 15 Machi 2021 baada ya kupokea malalamiko kuhusiana na matumizi pamoja na mipaka ya eneo hilo.

Waziri wa Ardhi Myumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiangalia wataalamu wa upimaji wakionesha mwisho wa mpaka wa moja ya nyumba katika mtaa wa Nzasa Kinondoni alipokwenda kutatua mgogoro wa ardhi baina ya wananchi wa mtaa huo tarehe 15 Machi 2021.


Akiwa katika eneo hilo, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alibaini uliukwaji wa mipaka ya maeneo hayo huku  baadhi ya wamiliki katika nyumba za mtaa huo wakiongeza ukubwa wa maeneo yao na kuingia sehemu ya barabarani kwa takriban mita nne na wengine wakiziba mifereji ya maji taka.

Waziri wa Ardhi Myumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akionesha mpaka wa moja ya nyumba zilizopo katika mtaa wa Nzasa kata ya Kijitonyama katika manispaa ya kinondoni alipokwenda kutatua mgogoro wa ardhi baina ya wananchi wa mtaa huo tarehe 15 Machi 2021.


Kufuatia hali hiyo, Waziri Lukuvi aliagiza ofisi ya ardhi mkoa wa Dar es Salaam pamoja na idara ya ardhi katika halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kuhakikisha inafufua mipaka ya maeneo hayo haraka ili kubaini wamiliki waliojiongezea maeneo kinyume na sheria.

“Uamuzi wangu baada ya kubaini ukiukwaji, timu ya wilaya na mkoa ije ifufue mipaka bila kubomoa nyumba na mjue ni kosa kujiongezea eneo. Ukimilikishwa jenga kwa mpango wa serikali siyo kujiamulia na heshimu mipaka ya serikali ” alisema Lukuvi.

Waziri wa Ardhi Myumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na wananchi wa mtaa wa Nzasa kata ya Kijitonyama katika manispaa ya kinondoni alipokwenda kutatua mgogoro wa ardhi baina ya wananchi wa mtaa huo tarehe 15 Machi 2021.


Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi, timu kutoka ofisi hizo mbili itakapoenda kufufua mipaka katika eneo hilo  itamuonesha kila mmiliiki eneo lake ambapo alisisitiza kuwa, baada ya kukamilika kazi hiyo kila mmiliki wa ardhi atatakiwa kubaki eneo lake kulingana na ukubwa wa kiwanja chake na maeneo ya barabara pamoja na njia za maji taka yaachwe wazi.

Waziri wa Ardhi Myumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na wananchi wa mtaa wa Nzasa kata ya Kijitonyama katika manispaa ya kinondoni alipokwenda kutatua mgogoro wa ardhi baina ya wananchi wa mtaa huo tarehe 15 Machi 2021.


“Lakini tushajua katika viwanja vyenu kuna walioongeza maeneo kwa madai kuwa ni maeneo ya wazi, msitamani vitu vya watu wengine ,mjenge kwa kuzingatia maeneo yanayowahusu na si vinginevyo. Alisema Waziri Lukuvi.


Baadhi ya wamiliki wa nyumba katika Mtaa huo wa Nazasa, kata ya Kijitonyama Manispaa ya Kinondoni walimueleza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa walifanya maamuzi hayo ya kuongeza maeneo bila kujua na kudhani maeneo hayo ni ya wazi na kumuomba Waziri Lukuvi kungalia namna ya kuwasaidia kwa kuwa wameshajenga katika maeneo hayo.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Mitazamo ya Uongozi ya Mhe. Ummy Ally Mwalimu katika Sekta za Afya, Maendeleo ya Jamii, na Haki za Watoto

Ummy Ally Mwalimu ameonyesha mitazamo ya uongozi yenye mwelekeo wa kujali maendeleo na ustawi katika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *