Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema kuwa serikali itakamilisha ujenzi wa kilometa 2,500 za lami na kuanza ujenzi wa barabara za lami zenye urefu wa kilometa 6,006.
Rais Magufuli amesema hayo wakati akifungua Bunge la 12 mjini Dodoma baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu Oktoba 2020, ambapo amesema kuwa anajua Wabunge wengi wametoa ahadi za barabara za lami kwenye maeneo yao.
Amesema kuwa ili kufikia lengo la kuunganisha Mikoa na Wilaya kwa Barabara za lami, barabara hizo zimetajwa kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2020- 2025 na kuongeza kuwa nyingine zinatokana na ahadi walizotoa katika kipindi cha Kampeni.
“Tumepanga pia kukamilisha ujenzi wa madaraja saba na kuanza madaraja mengine 14, ikiwemo daraja la Busisi, Wami na Pangani ” – amesema Rais Dkt. Magufuli.
Amesema serikili itaendelea kushughulikia tatizo la msongamano wa magari kwenye Miji na Majiji husasani Arusha, Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza na Dodoma ambapo wamepanga kujenga barabara ya mzunguko ya njia nne yenye urefu wa kilometa 110 katika Mkoa wa Dodoma ambapo Makandarasi wawili tayari wamekwi shapatikana na ujenzi utaanza hivi karibuni