SERIKALI ITAKAMILISHA UJENZI WA BARABARA KILOMETA 2,500 ZA LAMI – RAIS MAGUFULI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete mara baada ya kufungua Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma leo tarehe 13 Novemba, 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema kuwa serikali itakamilisha ujenzi wa kilometa 2,500 za lami na kuanza ujenzi wa barabara za lami zenye urefu wa kilometa 6,006.

Rais Magufuli amesema hayo wakati akifungua Bunge la 12 mjini Dodoma baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu Oktoba 2020, ambapo amesema kuwa anajua Wabunge wengi wametoa ahadi za barabara za lami kwenye maeneo yao.

Ad
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia pamoja na kulifungua rasmi Bunge hilo la 12 leo tarehe 13 Novemba 2020 jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameongozana na Spika wa Bunge Job Ndugai wakati akiingia ndani ya Bunge jijini Dodoma kwa ajili ya kuhutubia pamoja na kulifungua rasmi Bunge hilo la 12 leo tarehe 13 Novemba 2020.

Amesema kuwa ili kufikia lengo la kuunganisha Mikoa na Wilaya kwa Barabara za lami, barabara hizo zimetajwa kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2020- 2025 na kuongeza kuwa nyingine zinatokana na ahadi walizotoa katika kipindi cha Kampeni.

“Tumepanga pia kukamilisha ujenzi wa madaraja saba na kuanza madaraja mengine 14, ikiwemo daraja la Busisi, Wami na Pangani ” – amesema Rais Dkt. Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Gwaride la Heshma lililoandaliwa na Vikosi vya Jeshi la Polisi nchini mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma kwa ajili ya kuhutubia pamoja na kulifungua rasmi Bunge hilo la 12 leo tarehe 13 Novemba 2020.

Amesema serikili itaendelea kushughulikia tatizo la msongamano wa magari kwenye Miji na Majiji husasani Arusha, Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza na Dodoma ambapo wamepanga kujenga barabara ya mzunguko ya njia nne yenye urefu wa kilometa 110 katika Mkoa wa Dodoma ambapo Makandarasi wawili tayari wamekwi shapatikana na ujenzi utaanza hivi karibuni

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA ATEMBELEA RUKWA.. AANGAZIA AFYA, ELIMU, KILIMO NA MIUNDOMBINU KWA MIRADI YA MAENDELEO.

Katika ziara ya Rais Samia siku ya leo iliangazia kwenye sekta ya Afya, Elimu, Kilimo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *