TUMEPANGA KUNUNUA MELI NANE ZA UVUVI – RAIS DKT. MAGUFULI

Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema kuwa serikali imepanga kununua meli nane za uvuvi ili kuboresha sekta ya uvuvi ili kufikia bahari kuu.

Rais Magufuli amesema hayo wakati akifungua Bunge la 12 mjini Dodoma baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu Oktoba 2020, amesema kuwa meli hizo zitakazonunuliwa nne zitatumika Zanzibar na nne zitatumiwa Tanzania Bara.

Ad

“Kwa kushirikiana na shirika la IFAD, tumepanga kununua meli nane za uvuvi ambazo zitashiriki katika uvuvi wa bahari kuu katika upande wa Zanzibar na Tanzania Bara, tunakusudia kujenga bandari kubwa ya uvuvi itakayotoa ajira zipatazo 30,000 – Amesema Rais Magufuli

Aidha, amesema kuwa Serikali itakuza shughuli za uvuvi katika maziwa makuu na mito mikubwa, na kuhamasisha wavuvi wadogo kujiunga kwenye vikundi ili kuweze kuwapatia mitaji, ujuzi, vifaa na zana za uvuvi pia, na kupitia upya tozo na kuwapunguzia kero na kuvutia uwekezaji

Ad

Unaweza kuangalia pia

MWENDO KASI LEOTakwimu za Sasa za Utekelezaji wa Mradi wa Mwendo Kasi kwa Mwaka 2024

Mradi wa Mwendo Kasi (BRT) nchini Tanzania unaendelea kupiga hatua kubwa katika utekelezaji wake mwaka …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *