UFARANSA KUENDELEZA AWAMU YA TANO YA MRADI WA MABASI YA MWENDOKASI

Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini, Mhe. Manfredo Fanti akimuelezea jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimuelezea jambo Balozi wa Ufaransa hapa nchini, Mhe. Frederic Clavier wakati walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam

Serikali ya Ufaransa imeahidi kutoa Euro milioni 150 sawa na shilingi bilioni 413 kwa ajili ya kuendeleza mradi wa awamu ya tano wa ujenzi wa mradi wa mabasi ya mwendokasi jijini Dar es Salaam.

Ahadi hiyo imetolewa na Balozi wa Ufaransa hapa nchini, Mhe. Frederic Clavier wakati alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi, (Mb) katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Ad

Prof. Kabudi amesema kuwa mazungumzo yake na Mhe. Clavie yalijikita katika utekelezaji wa mambo waliyokubaliana wakati alipofanya ziara ya kikazi mwezi Februari nchini Ufaransa.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Msalaba Mwekundu: Nguzo ya Kibinadamu na Ujenzi wa Jamii Imara

Msalaba Mwekundu, ambao ni sehemu ya Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *