- Tanzania imetajwa kuweka historia katika tasnia ya madini baada ya Almasi yenye Karati 512.15 kupatikana hivi karibuni katika eneo la Maganzo Mkoani Shinyanga na kuuzwa kwa jumla ya shilingi Bilioni 3.2.
- Akizungumza katika mahojiano maalum kuhusiana na madini hayo,Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo amesema kuwa kutokana na kupatikana kwa almasi hiyo Serikali itapata mapato ya takribani shilingi milioni 235,000/- kama kodi na tozo mbalimbali ikiwemo mrabaha ambayo yamelipwa Serikalini baada ya mauzo hayo.
- Kuuzwa kwa jiwe hilo moja la almasi katika soko la madini mkoani Shinyanga ni muendelezo wa tija inayopatikana kupitia masoko hayo toka kuanzishwa kwake nchini,jumla ya shilingi bilioni 34.3 zimepatikana kwenye biashara ya dhahabu iliyofanyika katika kipindi cha mwezi mmoja tu kati ya Machi 17 mpaka Aprili 17 mwaka huu katika masoko ya madini kote nchini, kwa mujibu waziri wa Madini,Doto Biteko, aliyetoa taarifa hiyo hivi karibuni.
- “Natoa wito kwa wachimbaji wote,madalali na mawakala,kuyatumia ipasavyo masoko hayo kwakuwa kila mmoja atapata stahiki yake tofauti na awali kabla ya kufunguliwa kwa masoko hayo ambapo wachimbaji hawakuwa kwenye mikono salama kufutia kutokuwa na mfumo rasmi wa uuzaji madini yao”.Alisisitiza mhe. Nyongo
- Akifafanua amesema kuwa kila mchimbaji anapaswa kuzingatia sheria na Kanuni za sekta ya madini ili kuepuka mkono wa sheria na hatua nyingine ikiwa ni pamoja na kutaifishwa kwa madini yao pale watakapobainika kutaka kutorosha madini ama kujihusisha na magendo.
- Aliongeza kuwa baada ya kupatikana kwa almasi hiyo wataalamu wa Wizara hiyo walifanya tathmini ili kuona ubora wake na kiwango kilichopatikana ili kuhakikisha kuwa Serikali inapata mapato yake.
- “ Serikali ya Awamu ya Tano imeweka makazo katika kuimarisha sekta ya madini nchini ili itoe mchango unaostahili katika uchumi wetu ndio maana tunaona kuwa kupitia masoko ya madini tuliyoanzisha hata mchimbaji huyu aliyepata hii almasi pale Maganzo aliiuza kupitia soko letu la madini baada ya kufuata taratibu zote” alisisitiza Mhe. Nyongo
- Tanzani ni moja ya nchi zenye utajiri mkubwa wa madini ya aina mbalimbali ikiwemo Almasi, Tanzanite, Dhahabu na mengine mengi.
- Serikali ya Awamu ya Tano imeweka mkazo katika kuimarisha sekta ya madini ikiwemo kuimarisha taratibu za uuzaji wa madini yote yanayozalishwa hapa nchini, kuimarisha usimamizi, kuwawezsha wachimbaji wadogo ili waweze kuchimba kwa tija.Na Mwandishi Wetu
Ad