Matokeo ChanyA+

Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+.

Ni wajibu wenu kutumia utaalamu katika majukumu -Makamu wa Rais

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wanaotoa huduma katika sekta ya afya kutoa Huduma bora. Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa jengo la kituo cha Mama na Mtoto katika hospitali ya KMKM Kibweni ikiwa sehemu ya maadhimisho ya …

Soma zaidi »

NAIBU WAZIRI, KANYASU ATEMBELEA IHUMWA MJI WA SERIKALI KUKAGUA UJENZI JENGO LA MALIASILI NA UTALII

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu amesema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii linalojengwa ndani ya mji wa Serikali katika eneo la Ihumwa Jijini Dodoma. Ameyabainisha hayo wakati alipotembelea eneo hilo kwa ajili ya kukagua maendeleo yaliyofikiwa katika ujenzi …

Soma zaidi »

SERIKALI KUTUMIA SH.TRILIONI 1.3 KWA AJILI YA MIRADI YA MAJI MIJI 28 NCHI NZIMA-PROF. MKUMBO

Serikali inatarajia kutumia Shilingi Tirioni 1.3 kupitia mkopo toka Exim benki ya nchini India kwa ajili ya miradi mikakati ya maji katika Miji 28 nchi nzima ili kukabiliana na tatizo la maji. Hayo yamebaimnishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo alipofanya ziara  katika mamlaka ya Maji …

Soma zaidi »

SERIKALI YAZIPA KANDARASI YA THAMANI YA 2.9BN KAMPUNI ZA VIJANA KUTEKELEZA MAFUNZO YA KILIMO CHA KITALU NYUMBA

Serikali kupitia Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imezipa Kandarasi ya thamani ya shilingi 2.9 bilioni kampuni tatu za vijana wa Kitanzania ili kutekeleza mafunzo kwa wakufunzi ya kilimo cha Kitalu Nyumba (Green House). Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana …

Soma zaidi »

RAIS DKT. MAGUFULI ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MKATABA WA MAUZIANO YA MAHINDI KATI YA NFRA NA WFP IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 04 Januari, 2019 ameshuhudia utiaji saini wa mkataba wa mauziano ya mahindi kati ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Shirika la Chakula Duniani (WFP) uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam. Mkataba huo …

Soma zaidi »

BARABARA YA MBINGA-MBAMBA BEY KUKAMILIKA 2021

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekagua mradi wa ujenzi wa barabara ya lami kutoka Mbinga kwenda Mbamba bey yenye urefu wa kilomita 69 itakayogharimu sh. bilioni 129.3. Amekagua barabara hiyo leo (Ijumaa, Januari 4, 2019) wakati akielekea wilayani Mbinga akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi ya siku …

Soma zaidi »

DK. SHEIN AMEUFUNGUA UWANJA WA MICHEZO WA MAO TSE TUNG

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amekemea tabia iliojengeka nchini ya wanamichezo ku[peleka kesi za michezo mahakamani, na kusema hatua hiyo imekuwa ikidumaza maendeleo ya michezo nchini . Dk. Shein aliyasema hayo leo katika hafla ya uzinduzi wa Uwanja wa Mao Tse Tung …

Soma zaidi »

DAWASA YAKABIDHIWA JENGO, WATAKIWA KUFANYAKAZI KWA BIDII

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kusimamia miradi ya maji kwa umakini mkubwa. Amewataka DAWASA kuhakikisha kufikia 2020 asilimia 85 ya vijijini na asilimia 95 ya mijini inapata maji safi na salama. Mkumbo amesema hayo …

Soma zaidi »