Taarifa Vyombo vya Habari

UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI CHA KALENGE WAKAMILIKA

Wananchi wa kijiji cha Kalenge wilayani Uvinza wameishukuru kwa Serikali kukamilika ujenzi wa zahanati na hivyo kuwahepusha na vifo vitokanavyo na uzazi. Hayo yamebainishwa na wakazi wa eneo hilo wakati walipotembelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto-Idara Kuu Afya  Dkt. Zainab Chaula ambaye ameanza ziara ya …

Soma zaidi »

WANANCHI JIMBO LA MTERA WANUFAIKA NA MRADI WA MAJISAFI NA SALAMA

Serikali  imepongezwa kwa kuwezesha wananchi kufikiwa na huduma ya majisafi na salama baada ya miaka zaidi ya hamsini bila kuwepo kwa huduma hiyo katika eneo lao. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso mwishoni mwa wiki wakati akizindua mradi wa maji katika jijiji cha Makang’a, jimbo la Mtera …

Soma zaidi »

TANZANIA YATAKA AMANI KUPUNGUZA MZIGO WA WAKIMBIZI AFRIKA

Tanzania imetaka Umoja wa Afrika na Jumuiya za Kimataifa kuongeza jitihada na nguvu katika kuleta amani katika maeneo yenye migogoro Barani afrika hususani katika Nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ili kuipunguzia Tanzania mzigo wa wakimbizi ulioubeba kwa muda mrefu hivi sasa. Makamu wa Rais wa …

Soma zaidi »

MRADI WA BOMBA LA MAFUTA AFRIKA MASHARIKI SALAMA KWA MAZINGIRA – WAZIRI ZUNGU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Azzan Zungu hii leo ameshuhudia makabidhiano ya Cheti cha tathmini ya athari kwa mazingira kwa mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la afrika mashariki ikiwa ni hitimisho la ripoti ya Tathmini ya mazingira kwa Mradi wa …

Soma zaidi »

MAFINGA WAKABIDHIWA RASMI MAJENGO YALIYOPO KATA YA CHANGARAWE ILI KUYATUMIA KUWA KITUO CHA AFYA

  Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi amesema kuwa wameakabidhiwa rasmi majengo  yaliyopo katika Kata ya Changarawe,  ambayo yalikuwa yakitumiwa na Mkandarasi wa barabara ya Mafinga – Igawa ili yatumike Kama Kituo cha Afya. Mbunge huyo alitoa maombi ya kukabidhiwa majengo hayo kwa Rais Dkt. John Magufuli  wakati akitokea katika …

Soma zaidi »

MOI YALETA MITAMBO YA KISASA YA UPASUAJI UBONGO BILA KUFUNGUA FUVU

Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kwa dhati kuboresha Sekta ya Afya nchini na tayari imeleta mitambo ya kisasa ya Maabara ya upasuaji wa Ubongo bila kufungua fuvu (Angio Suite). Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Taasisi …

Soma zaidi »

SERIKALI MKOANI SHINYANGA YAKUSANYA  BILIOINI 1.5 KAMA KODI YA MRABAHA NA ADA YA UKAGUZI KUTOKA KWA WACHIMBAJI

Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Joseph kumburu amesema kuwa utaratibu mzuri uliowekwa kwenye usimamizi wa uzalishaji na biashara ya madini kwa wachimbaji wasio rasmi mkoani Shinyanga umepelekea Serikali kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 1.56 kama kodi ya mrabaha na ada ya ukaguzi kuanzia mwezi Mei, 2019 hadi …

Soma zaidi »

TRA – WAFANYABIASHARA MSIJIHUSISHE NA BIASHARA ZA MAGENDO

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara na wachuuzi wanaoishi jirani na fukwe za Bahari ya Hindi kutojihusisha na biashara za magengo kwani kufanya hivyo ni kuisababishia nchi kukosa mapato yake stahiki kutokana na wahusika wa biashara hizo kukwepa kulipa kodi. Akizungumza na wafanyabiashara hao katika fukwe za bahari za …

Soma zaidi »

NCHI ZA SADC ZATAKIWA KUTATHMINI UCHUMI WAKE BILA KUTEGEMEA MASHIRIKA YA KIMATAIFA PEKEE

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema kuwa nchi za Afrika hasa zilizopo chini ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) zinatakiwa kujitazama na kushauriana kuhusu mwenendo wao wa uchumi badala ya kuyaachia Mashirika ya Kimataifa pekee. Rai hiyo imetolewa Jijini Dodoma wakati wa …

Soma zaidi »