Taarifa ya Habari

OFISI YA RAIS – UTUMISHI WAKAMILISHA UJENZI WA OFISI YAKE KWENYE MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA

Waziri Mkuu Kassim M. Majaliwa amewapongeza viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa usimamizi mzuri uliopelekea kumalizika kwa ujenzi wa ofisi hiyo  kwa wakati iliyopo mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma. Pongezi hizo amezitoa alipotembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, …

Soma zaidi »

MAKAMBA-USHIRIKIANO NDIO NJIA MUHIMU KATIKA KUPATA TAKWIMU SAHIHI

Tanzania ili iweze kufikia hatima ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi, ofisi ya Taifa ya takwimu ishirikiane vyema na taasisi pamoja na mashirika ya utafiti katika kuhakikisha tafiti zinazofanyika zinatoa takwimu sahihi. Rai hiyo imetolewa  Jijini Dodoma na Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, …

Soma zaidi »

WANANCHI WALIOPISHA MRADI WA UJENZI WA KITUO CHA KUPOZA UMEME KIJIJI CHA KIDAHWE WATALIPWA FIDIA – WAZIRI KALEMANI

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, amesema kuwa wananchi waliopisha mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme katika Kijiji cha  Kidahwe wilayani Kigoma watalipwa fidia kabla ya ujenzi kuanza. Alisema hayo jana wakati za ziara ya kikazi wilayani Kigoma na Uvinza ambapo alikagua eneo kutakapojengwa kituo cha kupoza umeme …

Soma zaidi »

WAZIRI KALEMANI AKAGUA REA III WILAYANI,BUHIGWE NA KIGOMA VIJIJINI

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Kasulu, Kigoma Vijijini na Buhigwe mkoani Kigoma kwa lengo la kukagua mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) ambapo pia aliwasha  umeme katika baadhi ya Vijiji. Akiwa wilayani Kasulu, Dkt Kalemani alikagua kazi …

Soma zaidi »

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA NBC

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 26, Machi 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Ndugu Theobald Maingu Sabi ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi huyo amefika ofisini kwa Makamu wa Rais kwa lengo …

Soma zaidi »

TANZANIA IMEONGOZA KUVUTIA WAWEKEZAJI KATI YA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

UWEKEZAJI  Sekta ya Uwekezaji imeendelea kukua ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki ambapo ripoti mbalimbali za uwekezaji duniani zinaonesha Tanzania imeongoza kwa kuvutia uwekezaji kati ya nchi za Afrika Mashariki. Kwa mfano, Ripoti ya Uwekezaji ya Dunia ya mwaka 2018 inayotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara …

Soma zaidi »

WAZIRI KAMWELWE AWATAKA WATUMISHI SEKTA YA UJENZI KUONGEZA UBUNIFU

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, amewataka wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), kuongeza ubunifu na bidii katika kazi wanazozifanya ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayoendelea duniani. Mhandisi Kamwelwe, amesema kuanzia sasa wafanyakazi wa sekta hiyo wawekewe mkakati utakaowapa …

Soma zaidi »

UJENZI WA MZANI DAKAWA MKOANI MOROGORO UMEKAMILIKA KWA ASILIMIA 98

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeishauri Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), kujenga nyumba za watumishi kwenye mzani mpya unaojengwa Dakawa Mkoani Morogoro ili kuwapunguzia adha wafanyakazi watakaokuwa wakifanya kazi kituoni hapo. Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo …

Soma zaidi »