OFISI YA RAIS – UTUMISHI WAKAMILISHA UJENZI WA OFISI YAKE KWENYE MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA

  • Waziri Mkuu Kassim M. Majaliwa amewapongeza viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa usimamizi mzuri uliopelekea kumalizika kwa ujenzi wa ofisi hiyo  kwa wakati iliyopo mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma.
  • Pongezi hizo amezitoa alipotembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo kwenye mji wa serikali, eneo la Mtumba jijini Dodoma.
WAZIRI MKUU
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim M. Majaliwa akifurahia jambo mara baada ya kuzungumza na baadhi ya viongozi na watumishi wa umma kwenye mji wa serikali, mara baada ya kutembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.
  • Mhe. Majaliwa amesema kuwa, ameridhishwa na kiwango cha ujenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iliyojengwa ndani ya kipindi cha miezi mitatu na kwa gharama nafuu ya kiasi cha shilingi bilioni moja iliyotengwa na serikali.
  •  “Serikali imekuwa ikifuatilia hatua zote za ujenzi katika mji wa serikali ili kuhakikisha ujenzi unafanywa kwa viwango, na jengo la Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora limekuwa likienda vizuri sana katika hatua zote” amesema Mhe. Majaliwa.
WAZIRI MKUU
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim M. Majaliwa akizungumza na baadhi ya viongozi na watumishi wa umma kwenye mji wa serikali, mara baada ya kutembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.
  • Mhe. Majaliwa ameongeza kuwa, anatambua kwamba Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora imeshafanya uzinduzi wa jengo lake, jambo ambalo ni jema na limeonyesha namna ambavyo ofisi hiyo imetekeleza vema maelekezo ya serikali.
  • Aidha, Majaliwa ameweka bayana kuwa, uzinduzi rasmi wa Ofisi zote zilizojengwa kwenye mji wa serikali utafanywa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika tarehe rasmi atakayoipanga.
WAZIRI MKUU
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa  akiwa ndani ya ofisi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika  iliyopo kwenye mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma. Kulia kwake ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael.
  • Waziri Mkuu Majaliwa ametoa wito kwa ofisi hiyo kuboresha mandhari ya nje ya  ofisi ili iweze kupewa kipaumbele na serikali kuwa ofisi itakayotumika kwa ajili ya  uzinduzi wa ofisi zote  zilizojengwa kwenye mji huo wa serikali.
  • Naye, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa amemshukuru Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim M. Majaliwa  kwa kutenga muda wake kuitembelea Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora katika mji wa serikali, na kumshukuru kwa namna alivyowahimiza mawaziri kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa ofisi zao kwenye mji wa serikali ili ukamilike kwa wakati.
WAZIRI MKUU
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa akitoa neno la shukrani kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa, mara baada ya Mhe. Majaliwa kutembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.
  • Dkt. Mwanjelwa kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, amemuahidi Mhe. Majaliwa kuwa, ofisi yake itatekeleza maelekezo aliyoyatoa na itaendelea kutekeleza maagizo anayoyatoa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
  • Awali, Kaimu Meneja wa Wakala ya Majengo Tanzania (TBA), Bw. Herman Tanguye amesema kuwa, Wakala ya Majengo Tanzania imekamilisha ujenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa asilimia 99.5% kwa muda uliopangwa na kwamba hatua iliyobakia ni kukamilisha mandhari ya nje ya ofisi.
  • Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa ameitembelea Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi za serikali kwenye mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma, kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuzindua ofisi hizo rasmi hivi karibuni.
Ad

Unaweza kuangalia pia

SERIKALI KUTOINGILIA TAALUMA YA UKAGUZI WA HESABU ZA FEDHA

Serikali imeeleza kuwa haina mpango wa kuingilia taaluma ya ukaguzi wa hesabu nchini kwa kuondoa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *