WANANCHI WALIOPISHA MRADI WA UJENZI WA KITUO CHA KUPOZA UMEME KIJIJI CHA KIDAHWE WATALIPWA FIDIA – WAZIRI KALEMANI

  • Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, amesema kuwa wananchi waliopisha mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme katika Kijiji cha  Kidahwe wilayani Kigoma watalipwa fidia kabla ya ujenzi kuanza.
  • Alisema hayo jana wakati za ziara ya kikazi wilayani Kigoma na Uvinza ambapo alikagua eneo kutakapojengwa kituo cha kupoza umeme wa gridi ambao utatoka Tabora hadi Kigoma kwa msongo wa kV 132.
WAZIRI KALEMANI
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa pili kushoto) akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mwanamvua Mlindoko wakati alipofanya ziara ya kukagua kazi ya usambazaji umeme katika Kijiji cha Nyanganga wilayani humo.
  • “ Tunawapongeza wananchi kwa kupokea mradi huu kwa mikono miwili, lakini tunajua kuna wananchi wanaopaswa kulipwa fidia, ni haki yao ya msingi, hivyo hatutaweza kuanza ujenzi mpaka mtakapolipwa kwanza.” Alisema Dkt Kalemani.
  • Aliongeza kuwa, Serikali imetenga shilingi milioni 722 kwa ajili ya malipo ya fidia kwa wananchi na kwamba makadirio yameshafanyika na taratibu za uhakiki zinaendelea ili wananchi wapate kile wanachostahili.
WAZIRI KALEMANI
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa Tatu kutoka kulia) akizungumza na wanachi katika Kijiji cha Kidahwe wilayani Kigoma (hawapo pichani) wakati alipofika kijijini hapo kukagua eneo kutakapojengwa kituo cha kupoza umeme. Wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Samson Renard.
  • Alisema kuwa,  wananchi watakaopisha njia hiyo ya umeme pia watalipwa fidia na kwamba ujenzi utaanza wakati wowote baada ya malipo ya hayo kukamilika.
  • Akiwa wilayani Uvinza, Waziri wa Nishati alikagua kazi ya usambazaji umeme vijijini katika Kijiji cha Kazuramimba na Nyanganga ambapo mkandarasi kampuni ya CCCE Etern anaendelea na kazi.
WAZIRI KALEMANI
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa Tatu kutoka kushoto) akikagua miundombinu ya umeme katika Kijiji cha Kazuramimba wilayani Uvinza Mkoa wa Kigoma.
  • Katika Kijiji cha Kazuramimba alikuta mafundi wakiendelea na kazi ya ufungaji wa transfoma ambapo msimamizi wa mradi huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) alimweleza kuwa, kazi hiyo inakamilika tarehe 27 Machi, 2019 na baada ya hapo wataanza kuunganishia umeme wananchi.
  • Akiwa katika Kijiji cha Nyanganga, Dkt Kalemani alimwagiza mkandarasi kuhakikisha kuwa, Kijiji hicho kinapata umeme tarehe 31 Machi, 2019 ambapo pia aliiagiza TANESCO kutoa elimu kwa wananchi ili wahamasike kuunganisha umeme kwenye nyumba zao.
Ad

Unaweza kuangalia pia

UUNGANISHAJI UMEME VIJIJINI UENDE SAMBAMBA NA IDADI KUBWA YA KUWAWASHIA WATEJA

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amewaagiza Wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini(REA) pamoja …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.