MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA NBC

MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Ndugu Theobald Maingu Sabi (kushoto) mara baada ya mazungumzo ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam.
  • Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 26, Machi 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Ndugu Theobald Maingu Sabi ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam.
  • Mkurugenzi huyo amefika ofisini kwa Makamu wa Rais kwa lengo la kujitambulisha akiwa ameongozana na Meneja mahusiano na Serikali Bw. William Kalaghe pamoja na Afisa Masoko wa NBC Bi. Neemarose Singo.
MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Ndugu Theobald Maingu Sabi, Afisa Masoko wa NBC Bi. Neenarose Singo pamoja na Meneja wa Mahusiano na Serikali Ndugu William Kallaghe (kulia) mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Ad

Unaweza kuangalia pia

TANZANIA YATAKA AMANI KUPUNGUZA MZIGO WA WAKIMBIZI AFRIKA

Tanzania imetaka Umoja wa Afrika na Jumuiya za Kimataifa kuongeza jitihada na nguvu katika kuleta …

Oni moja

  1. pamoja sana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *