Maktaba Kiungo: WIZARA YA AFYA

MLOGANZILA IMEBORESHA HUDUMA KWA WANANCHI NA ITAENDELEA KUBORESHA ZAIDI – PROF.MAJINGE

Bodi ya Wadhamini, Hospitali ya Taifa Muhimbili imeupongeza Uongozi wa kwa kuboresha huduma za afya kwa wananchi katika Hospitali ya Mloganzila. Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Prof. Charles Majinge katika kikao cha kawaida cha Bodi hiyo kilichofanyika Hospitali ya Mloganzila ambapo Menejimenti iliwasilisha taarifa ya utendaji …

Soma zaidi »

WANANCHI WA MKOA WA PWANI WAPONGEZA UBORESHAJI HUDUMA ZA AFYA

Waganga, Wakunga na Wananchi wa Mkoa wa Pwani wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa hatua inazozichukua kuboresha huduma za Afya kwa kutoa fedha kwa ajili ya upanuzi wa vituo vya afya na ujenzi wa hospitali za Wilaya mkoani humo. Pongezi hizo zimetolewa na wadau hao wa afya mapema wiki hii, …

Soma zaidi »

MUHIMBILI YAFANYA UCHUNGUZI WA AWALI WA KUANGALIA UVIMBE KWENYE MATITI BILA KUFANYA UPASUAJI

Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) leo imetoa huduma ya uchunguzi wa awali wa kuangalia uvimbe kwenye matiti bila kufanya upasuaji. Akizungumzia zoezi hilo mtaalam wa Radiolojia wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila Dkt. Lulu Sakafu amesema katika zoezi hilo endapo mgonjwa …

Soma zaidi »

TAASISI YA (MOI) YAFANYA UCHUNGUZI WA KIBOBEZI WA MOYO KWA KUTUMIA KIPIMO CHA MRI (Cardiac MRI Contrasted study).

Taasisi ya Mifupa (MOI) kwa mara ya kwanza imefanya uchunguzi wa kibobezi wa moyo kwa kutumia kipimo cha MRI (Cardiac MRI Contrasted study). Kipimo hicho ambacho hakijawahi kufanyika katika Hospitali ya Umma hapa nchini kipimo hicho kinaonyesha vyumba, milango, mishipa ya damu na misuli kwa ufasaha mkubwa.

Soma zaidi »

WAGONJWA MOI KUFANYIWA UPASUAJI BILA NUSU KAPUTI

Taasisi ya tiba ya Mifupa MOI imeanzisha huduma ya kutoa dawa za usingizi (Reginal block Anaesthesia) ambapo eneo husika linalofanyiwa upasuaji ndilo litakolo husika kwa kuzuia mishipa ya fahamu na hivyo mgonjwa kuwa macho na kuzungumza au hata kusoma gazeti Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface …

Soma zaidi »

WAZIRI MKUU AKAGUA ENEO LA UJENZI WA HOSPITALI YA UHURU CHAMWINO

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekagua eneo la ujenzi wa hospitali ya Uhuru lenye ukubwa wa ekari 109 lililoko katika wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma. Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Maduma wilayani humo, Waziri Mkuu amesema uamuzi wa Serikali ya kijiji hicho wa kutenga maeneo ya maendeleo ni wa kupigiwa mfano …

Soma zaidi »

HOSPITAL YA KIBONG’OTO YAJIDHATITI KATIKA UTOAJI TIBA

Hospitali ya Magonjwa ambukizi Kibong’oto inayotoa huduma ya Kifua Kikuu ‘TB’ na magonjwa mengine ya kuambukiza hasa UKIMWI imeendelea kutoa huduma bora kutokana na serikali kuwekeza katika ununuzi wa vifaa vya kisasa vya uchunguzi na tiba. Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo Dkt.Riziki Kisonga wakati akizungumza na maofisa …

Soma zaidi »

MAABARA YA VINASABA VYA WANYAMA KUANZISHWA ARUSHA

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Kaskazini – Arusha, ipo mbioni kuanzisha Maabara maalum Vinasaba vya wanyama ambayo itasaidia kutambua asili ya mnyama ikiwemo wanyama waliopo ama waliokufa. Akizungumza wakati wa ziara maalum ya Maafisa Uhusiano waliotembelea Kanda hiyo leo, Meneja Kanda ya Kaskazini Christopher Anyango …

Soma zaidi »

TFDA NI YA KWANZA BARANI AFRIKA KWA MIFUMO BORA YA UDHIBITI

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imesema katika kipindi Cha Miaka mitatu imeweza kufanya mambo mbalimbali ya udhibiti wa usalama, ubora na usalama wa bidhaa za ndani na nje ya Nchi ikiwemo kutambulika kimataifa kwa kuzingatia  viwango vya Kimataifa vya ISO 9001: 2015. Hii ni kutokana na mafanikio ya miaka mitatu …

Soma zaidi »