IRINGA: Ziara ya Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe Ally Hapi yaibua makubwa

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi ameagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu na uchunguzi wa jinai kwa watendaji mbalimbali wa kijiji cha utosi, kata Sadani akiwemo katibu tarafa wa Sadani kwa makosa mbalimbali wanayotuhumiwa.

ALLY HAPPY IRINGA.jpeg

Katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi kijiji cha Utosi tarafa ya SADANI, wananchi wamedai viongozi hao kuwachangisha michango ya kujenga zahanati na daraja huku ikipita miaka kadhaa bila zahanati na michango yao kuyeyuka.
Aidha, wamewatuhumu viongozi hao kuwa wababe, wanaonyanyasa wananchi masikini, kuchukua rushwa na kuwatoza faini mbalimbali bila ya risiti na kupora haki za wasio na uwezo wa kutoa rushwa.

Ad

ALLY HAPPY IRINGA. 2

Hapi ameagiza mamlaka ya TAKUKURU na zile za nidhamu za katibu tarafa wa SADANI na watendaji wengine kuchukua hatua kali mara moja dhidi ya watendaji hao.

Mheshimiwa mkuu wa Mkoa, sisi tulishinda kesi baraza la kata Juu ya mtu mmoja mwenye pesa kuchukua ardhi yetu hapa kijijini. Lakini katibu tarafa huyu Mhagama alituita akasema yeye ndio mkuu wa migogoro ya ardhi hapa SADANI. Kwakua sisi ni masikini hatuna hela ya kumuhonga, akasema yule aliyeshindwa kesi ndiye anamoa haki na akatutisha tukiendelea kufuatilia suala hili atatuweka rumande.Tunaomba msaada wako,sisi ni masikini hatuna kitu, tunanyanyaswa tunatishwa.Yule tajiri anaendelea kulima shamba letu na hatuna pakwenda.Hata nakala ya hukumu hadi leo mwaka mzima tumenyimwa…”
Alieleza wananchi mmoja

ALLY HAPPY IRINGA. 1.jpeg

Katika mkutano huo uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Sadani katika tarafa ya Sadani wakati akisikiliza kero za wananchi wa eneo hilo ambapo ndugu Israel Mdulungwa mkazi wa kijiji cha Utosi alitoa kero yake ya wananchi kutozwa fedha kinyume na sheria na kutopewa risiti na mtendaji wa kijiji hicho Patrick Lakika ambapo RC Hapi amemtaka mtendaji huyo kuwalipa wananchi wote aliowachukulia fedha zao kinyume na sheria na kumtaka mkurugenzi wa halmashauri ya Mufindi kumkata kwenye mshahara wake na kuwalipa wananchi wanaomdai.

RC Hapi ameagiza kuchukuliwa hatua kali za kiutumishi na kijinai Afisa tarafa wa tarafa ya Sadani Christopher Mhagama iwe fundisho kwa watendaji wengine wa serikali.Aidha ameagiza Mwanasheria wa halmashauri kuhakikisha baraza la kata linawapa nakala ya hukumu na barua ya kukazia hukumu ili waweze kupata haki yao.

ALLY HAPPY IRINGA. 4.jpeg

Mkuu huyo wa mkoa ametembelea mradi wa tenki la kuhifadhia maji katika kijiji cha Maduma lenye ujazo wa lita laki moja ambao utahudumia zaidi wananchi 1626 katika vitongoji 4 uliotekelezwa na wizara ya maji wenye thamani zaidi ya shilingi milioni 73.

Mrafi mwingine ni wa ufugaji wa nyuki unaofanywa na mfugaji Meshack Nyika kwenye kata ya Igombavanu wenye mizinga 57 na kumkabidhi mizinga 10 ya kisasa ya kufugia nyuki ikiwa ni juhudi za mkoa huo kuwawezesha wananchi katika nyanja mbalimbali na kuahidi kuwapeleka baadhi ya wafugaji nyuki mkoani humo kwenye shamba la ufugaji nyuki la Waziri Mkuu mkuu mstaafu Mizengo Pinda ili waweze kujifunza kuzalisha asali nyingi kwenye eneo dogo kwa mfumo wa kisasa.

Kwenye mradi wa lambo la kunyweshea mifugo na kilimo cha matikiti maji ambao umegharimu shilingi milioni 2.8 unaohudumia zaidi ya kaya 106 na kilimo cha umwagiliaji cha matikiti maji zaidi ya hekari 23, amewataka wananchi walio karibu na lambo hilo kutunza mazingira ili liendelee kuwafaidisha.
RC Hapi ameweza kuchangia shilingi laki 5 katika ujenzi wa mabweni wa shule ya sekondari Mgalo ambayo yanajengwa kwa kwa nguvu za wananchi na kuwapongeza wananchi wa kata hiyo ya Sadani kwa juhudi zao za kuleta maendeleo wakati alipotembelea na kukagua ujenzi huo.

Wakati anawahutubia wananchi RC Hapi amesema Rais Magufuli amemtuma kuwatumikia wananchi wa Iringa na kuhakikisha kero zao zinatatuliwa.
Ziara Iringa Mpya tarafa kwa tarafa

Ad

Unaweza kuangalia pia

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdory Mpango, tarehe 01 Novemba 2024 ameungana na kuongoza Waombolezaji Katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo,jijini Dar-es-Salaam, kuaga mwili wa marehemu Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali David Bugozi Musuguri

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *