Eng. Patrick MFUGALE aongelea kuanza kutumika Kwa Flyover kabla ya uzinduzi.

Barabara za juu katika eneo la Tazara jijini Dar es Salaam nchini Tanzania  zimeanza kutumika hii leo kwa majaribio ambapo uzinduzi rasmi utafanyika baada ya tarehe rasmi kupangwa.

Akizungumza mara baada ya kufanyika kwa uzinduzi huo wa majaribio injinia Patrick Mfugale ambaye barabara hizo zimepewa jina lake Mfugale Fylover amesema kuwa hatua hiyo imepunguza foleni kwa kiasi kikubwa

Hata hivyo kituo cha abiria kilichohamishwa kimeleta usumbufu kwa wananchi

Akifafanua kuhusu  vituo vya kushusha abiria injinia Mfugale amesema vituo rasmi katika eneo la Tazara vitapangwa vizuri baadaye.

Wananchi nao wamepongeza juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt John Pombe Magufuli

 

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha mazingira ya ufanyaji biashara za huduma za kifedha ili kuvutia uwekezaji wa ndani na nje kwa kuwa maendeleo endelevu ya taifa hayawezi kufikiwa bila ushiriki thabiti wa sekta binafsi

Amesema kuwa sekta ya fedha ni kichocheo kikubwa katika ukuaji wa Uchumi na ustawi wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *