SADC na MSD wafanikiwa kusaini mkataba utakaoipa mamlaka Bohari ya dawa nchini kuwa mnunuzi mkuu wa dawa, vifaa tiba na vitendanidhi vya maabara kwaajili ya nchi wanachama wa jumuiya ya SADC

MSD SASA KUNUNUA, KUSAMBAZA DAWA KWA NCHI ZOTE ZA SADC!

 

MKURUGENZI MKUU WA BOHARI YA DAWA(MSD) NA KATIBU MTENDAJI WA SEKRETARIETI YA SADC
Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya SADC Dkt.Stergomena L. Tax na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Ndugu Laurean Rugambwa Bwanakunu siku ya jumanne tarehe 09 Oktoba, 2018 – jijini wakiwa wanasaini mkataba wa makubaliano unaoipa mamlaka MSD kuwa ndiye mnunuzi mkuu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa ajili ya nchi 16 wanachama wa SADC – JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA.

Katibu Mtendaji wa Sekretariet ya SADC Dkt. Stergomena L. Tax na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu wamesaini mkataba wa makubaliano ya MSD kuwa mnunuzi Mkuu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa ajili ya nchi 16 wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

TUMEFANIKISHA
Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya SADC Dkt. Stergomena L. Tax akipongezana huku akibadilishana mikataba walioisaini na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Bwn. Laurean Bwanakunu katika hafkla ya kusaini mkataba wa SADC na MSD unaoipa mamlaka MDS kuwa mnunuzi mkuu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa ajili ya kuhudumia nchi zote za SADC.

Hatua hii inafuatia uteuzi wa serikali ya Tanzania kupitia Bohari ya Dawa (MSD) ulifanywa wakati wa mkutano wa SADC wa mawaziri wa Afya wa nchi wanachama, uliofanyika mwezi Novemba, 2017 nchini Afrika Kusini.

Ad
MSD ILIPOTEULIWA NA MAWAZIRI WA AFYA WA SADC
Novemba mwaka 2017, Mawaziri wa Afya wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Africa (SADC) kwa kauli moja walipitisha uteuzi wa nchi ya Tanzania kupitia Bohari ya Dawa (MSD) kuwa Mnunuzi Mkuu wa Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara kwa ajili ya nchi hizo kupitia mfumo wa Ununuzi Shirikishi (SADC Pooled Procurement Services (SPPS).

 

Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bw. Laurean Bwanakunu amesema tangu wakati huo hadi sasa wamekuwa wakishirikiana na na Sekretarieti ya (SADC) kuandaa rasimu ya mpango wa utekelezaji wa manunuzi ya pamoja yaani SADC Pooled Procurement Services (SPPS).

DKT. STERGOMENA L. TAX
Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya SADC Dkt. Stergomena Tax akizungumza wakati wa utiaji saini mkataba huo na kusema kuwa hii ni heshima kubwa sana kwa Tanzania.

Amesema kulingana na mpango huo, uratibu wa manunuzi unaanza rasmi tarehe leo, tarehe 9/10/2018, kupitia mkataba wa makubaliano yaani Memorandum of Understanding (MoU) kati ya MSD na Sekretarieti ya SADC.

Bwanakunu ameongeza kuwa MSD itakuwa na majukumu ya kupokea mahitaji ya manunuzi ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kutoka kwa nchi hizo 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), kununua dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara, kusimamia takwimu na taarifa za dawa pamoja na kusimamia Kanzidata (Database) ya dawa za nchi hizo.

Ameongeza kuwa MSD itasimamia bei elekezi ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara, kusimamia mfumo wa manunuzi kwa njia ya mtandao kwa nchi zote wanachama, kutoa huduma za kitaalam na kupanga bei elekezi.

MSD pia itaanzisha kitengo maalumu ndani ya kurugenzi ya manunuzi kwa ajili ya kazi hii ya ununuzi wa dawa, vifaa tiba ba vitendanishi vya maabara kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC tu.

PICHA YA PAMOJA
Picha ya pamoja baada kati ya Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya SADC na ujumbe wake pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa MSD akiwa na wafanyakazi wa Bohari hiyo

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Sekretariet ya SADC Dkt. Stergomena L. Tax ameeleza kuwa Tanzania kuwa mnunuzi mkuu wa dawa kwa nchi za Ukanda wa SADC ni heshima kubwa kwa Taifa, kuaminiwa kwa huduma bora, uwezo na kukidhi vigezo vya kitaalamu katika mnyororo wa ugavi.

ASANTE SANA
Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwn. Laurean Bwanakunu na Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya SADC Dkt. Stergomena L. Tax wakipongezana mara baada ya kumaliza shughuli ya utiaji saini mkataba unaoipa mamlaka MSD kuwa mnunuzi mkuu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa ajili ya nchi 16 za SADC. Wanao washuhudia kwa karibu pichani mmoja wao ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepi (wa kwanza kulia)

Makubaliano hayo yameshuhudiwa na Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye amesema kwamba SADC imeipa Tanzania heshima kubwa na kuichagiza MSD kuhakikisha inatekeleza majukumu yake vizuri ili isionekane kuwa SADC ilifanya makosa kuichagua Tanzania.

 

#SisiNiTanzaniaMpyA+

Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI UMMY AWATAKA WAZAZI KUWEKEZA KATIKA AFYA ZA WATOTO

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewataka wazazi kuwekeza …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *