Rais Dkt John Pombe Magufuli akipata chakula cha mchana na wachezaji wa Taifa Stars na viongozi wa michezo Ikulu jijini Dar leo Ijumaa Oktoba 19, 2018

Ni Lazima Mshinde! – Rais Magufuli

MOJA YA KAULI ZA MHE. RAIS KWA WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA
Tweet inayoonyesha kauli ya Mhe. Rais Magufuli katika hotuba yake alipokuwa akizungumza na wachezaji wa timu ya Taifa na viongozi wa TFF.
  • Rais  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wachezaji wa timu ya soka ya Taifa (Taifa Stars) kuongeza juhudi za kupata ushindi katika michuano mbalimbali inayoshiriki ikiwemo ya kufuzu fainali za michuano ya Afrika (AFCON) itakayofanyika mwakani nchini Cameroon.
USHINDI NI LAZIMA
Tweet; Mhe.Rais Magufuli akitoa Tshs. Mil. 50 kwaajili ya kusaidia maandalizi ya michezo iliyobaki ya timu ya Taifa ili iweze kufuzu katika fainali za Kombe la Afrika mwakani nchini Cameroon.
  • Mhe. Rais Magufuli amesema hayo leo alipokutana na kuzungumza na wachezaji wa Taifa Stars na viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  • Mhe. Rais Magufuli ambaye amechangia Taifa Stars shilingi Milioni 50 na baadaye kula chakula cha mchana na wachezaji hao, amesema kiu yake na kiu ya Watanzania ni kuona timu yao inapata ushindi na kuitangaza vyema Tanzania kimataifa na kwamba matokeo mabaya ya timu hiyo hukatisha tamaa.
  • “Wanangu nawapenda nendeni mkashinde, nendeni mkapeperushe vizuri bendera ya Tanzania, lengo letu iwe ni kushinda tu” amesema Mhe. Rais Magufuli.
RAIS MAGUFULI AKITOA PESA MILLION 50 KWA TIMU
Rais Dkt John Pombe Magufuli akikabidhi shilingi milioni 50 taslimu kwa ajili ya Taifa Stars kwa Waziri Dkt Harrison Mwakyembe, viongozi wa TFF na nahodha msaidizi wa Taifa Stars Erasto Nyoni alipokutana nao Ikulu jijini Dar leo Ijumaa.
  • Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameelezea kusikitishwa kwake na vitendo vya matumizi mabaya ya fedha, rushwa na uongozi mbaya katika vyama vya michezo hali iliyosababisha TFF kunyimwa fedha za ruzuku kutoka Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) na amewataka viongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, TFF na BMT kushugulikia dosari hizo ili Tanzania iendelee kupata ruzuku hiyo.
  • “Nawapa shilingi Milioni 50, nataka zikatumike kuimarisha timu na sio kunufaisha viongozi, na hizo fedha tunazonyimwa na FIFA fuatilieni kwa pamoja tuzipate ili zitusaidie kuendeleza timu zetu” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

VIJANA WAWE IMARA KULIPAMBANIA TAIFA

  • Pia amewataka wachezaji kujenga umoja wanapochezea timu ya Taifa na kutanguliza mbele maslahi ya Taifa badala ya maslahi ya timu zao, na amewasihi viongozi kutoingilia majukumu ya mwalimu wa timu ili aweze kuipanga timu yake kitaalamu kadiri atakavyoona inafaa kupata ushindi.
RAIS MAGUFULI AKIPOKEA JEZI
Rais Dkt John Pombe Magufuli akishukuru baada ya kupokea zawadi ya jezi toka kwa nahodha msaidizi wa Taifa Stars Erasto Nyoni alipokutana nao pamoja na viongozi wa michezo Ikulu jijini Dar leo Ijumaa
  • Katika maelezo yake Rais wa TFF Bw. Wallace Karia amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kukutana na wachezaji wa Taifa Stars na amemueleza kuwa TFF imejipanga kushirikiana na wadau kuhakikisha timu hiyo inafuzu kucheza AFCON mwakani nchini Cameroon, na pia ameeleza kuwa juhudi kama hizo zinafanywa kwa timu nyingine za Taifa zinazojiandaa kwa michuano ya kimataifa ambazo ni Serengeti Boys, Ngorongoro Heroes, Kilimanjaro Heroes na Twiga Stars.
  • Kocha Mkuu wa Taifa Stars Bw. Emanuel Amuneke amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kupata heshima ya yeye na wachezaji wake kukutana nae na amemhakikishia kuwa Taifa Stars ina wachezaji wazuri na wenye uwezo wa kushinda, na kwamba ana imani kuwa kwa michuano iliyobaki itafanikiwa kupata tiketi ya kushiriki AFCON mwakani.
Rais Dkt John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya jezi toka kwa nahodha wa Taifa Stars Erasto Nyoni
Rais Dkt John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya jezi toka kwa nahodha wa Taifa Stars Erasto Nyoni alipokutana nao pamoja na viongozi wa michezo Ikulu jijini Dar leo Ijumaa
  • Katika maelezo yake Rais wa TFF Bw. Wallace Karia amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kukutana na wachezaji wa Taifa Stars na amemueleza kuwa TFF imejipanga kushirikiana na wadau kuhakikisha timu hiyo inafuzu kucheza AFCON mwakani nchini Cameroon, na pia ameeleza kuwa juhudi kama hizo zinafanywa kwa timu nyingine za Taifa zinazojiandaa kwa michuano ya kimataifa ambazo ni Serengeti Boys, Ngorongoro Heroes, Kilimanjaro Heroes na Twiga Stars.
  • Kocha Mkuu wa Taifa Stars Bw. Emanuel Amuneke amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kupata heshima ya yeye na wachezaji wake kukutana nae na amemhakikishia kuwa Taifa Stars ina wachezaji wazuri na wenye uwezo wa kushinda, na kwamba ana imani kuwa kwa michuano iliyobaki itafanikiwa kupata tiketi ya kushiriki AFCON mwakani.

Kwa kufuatilia zaidi mkutano wa Rais Magufuli na Wachezaji wa timu ya Taifa

Ad

Unaweza kuangalia pia

BANDARI YA DAR ES SALAAM INAPANUKA NA KUIMARIKA: HATUA MUHIMU KWA UCHUMI WA TANZANIA

Bandari ya Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha biashara na uchumi wa Tanzania, na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *