SERIKALI YAANZA MAZUNGUMZO NA UJERUMANI YA MGAO WA MAPATO YATOKANAYO NA MJUSI MKUBWA ‘DINOSAUR’ KUPITIA WATALII

  • Serikali ya Tanzania kupitia Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga  imesema ipo kwenye hatua za awali za mazungumzo na Serikali ya Ujerumani kuona jinsi itakavyofaidika na mapato yatokanayo na utalii  kupitia mabaki ya Mjusi mkubwa ‘’Dinosaurs ambaye ni kivutio cha kikubwa cha  utalii  katika jumba la  Makumbusho nchini Ujerumani
  • Mjusi huyo kwa jina la kitaalamu anaitwa Dinosaur ambapo mabaki yake yalivumbuliwa  miaka  100 iliyopita katika eneo la Tendaguru  mkoani Lindi, yalikusanywa na kupelekwa  nchini Ujerumani ambako wataalamu waliyaunda na kisha kuyaweka kwenye Makumbusho hiyo.
  • Amesema lengo la mazungumzo hayo ni kutaka  kujua kiasi gani  cha mapato yanayokusanywa na  namna gani  wanavyoweza kugawana mapato hayo   yatokanayo na watalii kupitia mjusi huyo baina ya Serikali hizo mbili.
  • Amesema mwelekeo wa  mazungumzo hayo yaitapelekea Serikali ya Tanzania kufanya uamuzi   wa kumrudisha mjusi huyo  au kumuacha kule kule   lakini akiwa  analiingizia pato taifa
MABAKI YA MJUSI MKUBWA
Mabaki ya Mjusi mkubwa ‘’Dinosaurs ambaye ni kivutio cha kikubwa cha  utalii  katika jumba la  Makumbusho nchini Ujerumani
  • Ameyabainisha hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na mIkakati ya  Serikali ya kuendeleza vivutio vya utalii kwa mikoa ya Kusini.
  • Hata hivyo, Mhe.Hasunga amesema  uamuzi wa kumrudisha  mjusi huyo nchini utakuwa mgumu kwa vile sehemu kubwa ya mjusi huyo ameunganishwa unganishwa kwa kutumia vifaa maalumu.
  • Ameongeza kuwa kutokana na jinsi alivyounganishwa unganishwa na anakadiri wa kuwa na  urefu wa mita 13.7 kwenda juu  hivyo kumsafirisha itakuwa ngumu.
  • Katika hatau nyingine, Mhe Hasunga amesema hadi hivi sasa  Serikali ya Ujerumani haijaweza kuweka bayana kiasi cha mapato yanayokusanywa  kupitia Mjusi huyo licha ya kuwa Serikali hiyo  imekuwa ikifadhili miradi mingi ya uhifadhi nchini.
  • “Tunaamini kuwa pesa wanazofadhili miradi mingi ya Uhifadhi imekuwa inatokana na makusany okupitia Mjusi huyo Mkubwa” amesema Hasunga
  • Hata hivyo,kuendelea kuwepo kwa masalia ya mjusi huyo katika Makumbusho hiyo kuna manufaa makubwa kwa vile anatambuliwa kuwa ni wa kutoka Tanzania,Hivyo ni Balozi wa Utalii na utafiti wa kisayansi anayeitangaza Tanzania sehemu mbalimbali duniani.
Ad

Unaweza kuangalia pia

Benki ya NMB Tanzania yapongezwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

kwakuwa Kinara katika utendaji wake, kutengeneza faida kubwa ya mfano wa kuigwa na mashirika na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *