Bi. MKAPA – Tunaliondoa shirika la NIC katika utaratibu wa ubinafsishaji

  • Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuliimarisha Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwa kuliondoa katika utaratibu wa ubinafsishaji ambao uliwekwa awali.
  • Hayo yamebainishwa na  Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi Susana Mkapa, kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa tisa wa baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Bima la Taifa  Jijini Dodoma.
  • Bi Susana alisema kuwa, hatua za kuliondoa Shirika la NIC katika utaratibu wa ubinafsishaji zimefikia hatua nzuri ambapo utahitimishwa kwa kuandaa hati ya kisheria.
BI SUSAN MAKAPA
Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi Susana Mkapa
  • “Wizara ya Fedha na Mipango imeongeza muda wa mikataba ya kazi kwa watumishi kwa miezi mitatu, hivyo mawasiliano rasmi kuhusu mikataba hiyo yatafanyika, nawaomba watumishi muendelee kufanya kazi na kuwajibika wakati taratibu hizi za kuliondoa Shirika katika ubinafsishaji zikikamilika”. Alieleza Bi. Mkapa.
  • Vilevile alisema kuwa, maamuzi ya Mashirika na Taasisi za Serikali kupata huduma za Bima kupitia Shirika la Bima la Taifa ni ya Kisera na yanahusisha mamlaka mbalimbali, hivyo amelitaka Shirika hilo liendelee kufanya kazi kwa ushindani, kuongeza ufanisi, ubunifu na kuondokana na fikra za kufanyakazi kwa mazoea.
  • Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Bw. Sam Kamanga alisema kuwa baadhi ya Taasisi na Mashirika ya Umma yanasita kutumia Bima za Shirika hilo kwa kuwa hakuna tamko rasmi ambalo linasimamia utekelezaji hivyo kuiomba Serikali  kutoa tamko hilo.
  • Pia ameiomba Serikali kuliongezea Shirika hilo mtaji kwa kuwa uliopo wa kiasi cha Sh. bilioni 2.9, ni mdogo na haukidhi katika kuimarisha Shirika hilo kwa utoaji wa bidhaa mbalimbali kulingana na uhitaji wa Soko.
  • Naibu Katibu Mkuu Bi Susan Mkapa alilipongeza Shirika la NIC kwa kuwa na Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi ambao utekelezaji wa matakwa ya sheria na kanuni zinazosimamia mahusiano kazini kati ya Menejimenti na wafanyakazi, na ushirikishwaji katika uendeshaji wa Taasisi, hivyo akawataka watumishi hao kuhakikisha wanatoa ushauri utakao imarisha taasisi hiyo na kusaidia kufanikisha malengo ya maendeleo ya Taifa.
Ad

Unaweza kuangalia pia

Mitazamo ya Uongozi ya Mhe. Ummy Ally Mwalimu katika Sekta za Afya, Maendeleo ya Jamii, na Haki za Watoto

Ummy Ally Mwalimu ameonyesha mitazamo ya uongozi yenye mwelekeo wa kujali maendeleo na ustawi katika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *