MafundI na wahandisi wakiendelea na Kazi za ukarabati wa machine na mitambo katika kituo cha kupoza na kusambaza Umeme cha Mwakibete jijini Mbeya.

Kalemani: Vituo vya kupooza na kusambaza Umeme vifanyiwe ukaguzi kila siku

  • Mameneja wote wanaosimamia vituo vya kupoza na kusambaza umeme nchini wametakiwa kufanya ukaguzi ( checkup) wa kila siku asubuhi katika mitambo na mashine zilizopo katika vituo hivyo kuondoa adha ya kukatika umeme kutokana na hitilafu au uharibifu katika vituo hivyo.
  • Licha ya kuwa vituo hivyo vinafanyiwa ukarabati na ukaguzi wa kila mara au hata baada ya miezi kulingana na utaratibu waliojiwekea.
MATAGA---124Waziri wa Nishati, Dk.Medard Kalemani,
Waziri wa Nishati, Dk.Medard Kalemani, (katikati) akipita katika mitaa ya kijiji cha Nsalaga kukagua Miundombinu ya usambazaji wa huduma ya Umeme, unaotekelezwa na Shirika la Umeme, nchini (Tanesco) ambapo ametoa siku 14,kwa wananchi hao kuunganishwa na huduma hiyo.
  • Hayo yameleezwa na Waziri wa Nishati ,Dkt. Medard Kalemani , wakati wa ziara yake ya kikazi katika Jiji la Mbeya, baada ya kutembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Mwakibete na kukagua miradi ya kusambaza umeme katika kijiji cha Nsalaga na Iduda inayotekelezwa na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO).
  • Alieleza kuwa kumekuwa na changamoto ya kukatika umeme kwa muda mchache katika baadhi ya maeneo na sababu kuu ya ikielezwa kuwa ni hitilafu katika vituo au kuharibika kwa kifaa katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme.
  • Alifafanua kuwa changamoto hiyo inaepukika na kutoweka kabisa endapo wahandisi na mafundi watakuwa na tabia ya kufanya uchunguzi wa mitambo na mashine zao kila siku asubuhi kubaini tatizo kabla ya kutokea.
  • “ Mafundi na wahandisi muwe na tabia ya kufanya ukaguzi na matengenezo ya kila siku asubuhi badala ya kusubiri tatizo litokee, achene kufanya kufanya ukaguzi na matengenezo kwa mazoea, hii itasaidia kufahamu mapema tatizo linazoweza kutokea baadaye na kuondoa usumbufu wa kukatika umeme kwa wananchi hali ya kuwa kuna umeme mwingi nawa kutosha”, alisisitiza Kalemani.
  • Alifafanua kuwa kwa sasa serikali haitaki kuona mtu yeyote anakosa huduma ya umeme kwa muda Fulani kwa sababu tu kumetokea ya hitilafu katika mitambo na mashine katika vituo vya kupoza na kusambaza umeme, badala yake inataka umeme upatikane saa 24 na siku saba kwa wiki kwa kuwa umeme upo wa kutosha na ziada.
Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani
Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani (katikati mwenye kipaza sauti) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Iduda, ambao bado hawajaungwanishwa na huduma ya Umeme Licha ya miundombinu kuwafikia.
  • Aidha alisisitiza kuwa , pia Serikali haitaki kuona mwananchi wake anaingia gharama ya kutumia jenereta kwakuwa nchi inazalisha umeme mwingi, pia inataka kuondokana na matumizi ya majenereta kwa kuimarisha njia ya usafirishaji, usambazaji pamoja na uzalishaji wa umeme nchini
  • “Mpango wa serikali ni kuachana na matumizi ya magenereta kwa watu wote, wakiwemo wafanyabiashara, Makampuni, Mashirika na pia kuwapunguza gharama za maisha na kurahisisha utendaji wa kazi kuwa na umeme mwingi, wakutosha na ziada”, alisema Kalemani.
  • Hata hivyo alisema kuwa ni lazima katika kila kituo cha kupooza na kusambaza umeme kiwe na stoo ya kuhifadhi vifaa vya dharura vitakavyotumika endapo ikatokea kifaa kimeharibika au kupata hitilafu.
  • Alisisitiza stoo hizo ni lazima ziwe na vifaa vizima na vya kutosha wakati wote, badala ya vifaa hivyo kuhifadhiwa katika ofisi za mameneja wa kanda au mikoa, hivyo kuleta usumbufu pindi tatizo linapotokea.
Waziri wa Nishati, Medard Kalemani akikagua miundombinu
Waziri wa Nishati, Medard Kalemani akikagua miundombinu ya kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mwakibete, Jijini Mbeya na kuagiza mafundi na wahandisi katika Vituo vyote nchini kufanya ukaguzi wa kila siku kuepusha kukatika Umeme kutokana na hitilafu zinazojitokeza katika Vituo hivyo.
  • Akizungumzia huduma ya umeme wa viwandani, Dk. Kalemani alisema kuwa viwanda vikubwa vipewe umeme wa peke yao wa kutosha na uhakika ili wazalishe kwa wingi waweze kulipa kodi za na kuiingizia nchi mapato.
  • Alisema kwa kufanya hivyo kutaweza kuwabana wenye viwanda waokwepa kulipa kodi kwa kisingizo cha kutozalisha kutokana na kukosa huduma ya umeme.
  • Hivyo ametoa siku 10, kwa Tanesco, kufunga huduma ya umeme wa peke yake kwenye kiwanda cha kuzalisha saruji cha Mbeya, ili kiweze kuajiri watu na wengi zaidi, kuzalisha kwa wingi na kulipa kodi za serikali.
  • Katika hatua nyingine ametoa siku 14, kwa Tanesco kuhakikisha kuwa wanawaunganisha huduma ya umeme wakazi wa Kijiji cha Nsalaga na Iduda waliokidhi vigezo vya kupata huduma hiyo.
  • Alitolea ufafanuzi kuwa wananchi hao waunganishiwe huduma hiyo kwa gharama ya shilingi 27,000 tu, tofauti na gharama za Tanesco kwa kuwa vijiji hivyo vipo pembezoni mwa jiji la Mbeya, hali ya kuwa vinaoneka vipo mjini.
  • Akizungumzia kituo cha kuzalisha umeme cha jijini mbeya, Dk.Kalemani alisema ,kituo hicho kinauwezo wa kuzalisha megawati 130, ambapo mahitaji ya Mkoa mzima wa Mbeya, Songe pamoja na Makete ni Megawati 52, hivyo kunaziada ya megawati 78, hivyo wananchi wachamkie fursa ya kuunganishwa na huduma ya umeme.
Ad

Unaweza kuangalia pia

TPDC YAOKOA TRILIONI 12.7 KUAGIZA MAFUTA NJE YA NCHI

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika kipindi cha miaka minne ya Uongozi wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *