HOSPITAL YA TAIFA MUHIMBILI WAANZA ZOEZI LA KUPANDIKIZA VIFAA VYA USIKIVU KWA WATOTO

  • Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),leo  Novemba 12, 2018 wameanza zoezi upasuaji wa kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto 10 ambao wana matatizo ya kusikia baada ya kukamilika kwa maandalizi, mwisho zoezi hilo linafanyika hadi  hadi November 16, 2018.

    Watoto hao watapandikizwa vifaa vya usikivu baada ya wataalam kuwafanyia uchunguzi wa kina pamoja na wazazi kupatiwa ushauri wa kitaalamu. Baada ya watoto hao 10 kupandikizwa vifaa vya usikivu, jumla ya watoto watakaokuwa wamepandikizwa vifaa hivyo itafikia 21 tangu kuanza kwa upasuaji huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

BAADHI YA MADAKTARI
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Masikio, Pua na Koo kutoka nchini Misri, Prof. Lobna El Fiky akijadili jambo kwenye kikao cha maandalizi ya kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto wenye matatizo ya kusikia.
  • Daktari Bingwa wa upasuaji wa Masikio, Pua na Koo wa hospitali hiyo Dkt. Edwin Liyombo amesema maandalizi kwa ajili ya kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto hao yamekamilika.

    Dkt. Liyombo amesema kwamba walifanya kikao cha pamoja na wazazi wa watoto hao kwa ajili ya kuwaandaa na kuwapatia maelekezo jinsi ya kuwa karibu zaidi na watoto hao ili waweze kusikia vizuri na kuzungumza baada ya kupandikizwa vifaa vya usikivu.

WAZAZI NA MADAKTARI
Kulia ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Masikio, Pua na Koo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Shaban Mawalla akitoa taarifa ya mmoja wa watoto wenye tatizo la usikivu kwenye kikao hicho. Katikati ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Masikio, Pua na Mkoo wa Muhimbili, Dkt. Edwin Liyombo, mtaalam wa usikivu, Fayaz Jaffer na kushoto ni wazazi wakiwa kwenye kikao hicho.
  • “Wazazi wanatakiwa kuwafutilia kwa karibu watoto baada ya kupandikizwa vifaa vya usikivu. Zinahitajika nguvu za ziada ili watoto waweze kuzungumza vizuri na kusikia,” amesema Dkt. Liyombo.

    Katika mkutano huo wazazi wa watoto hao wameonyesha imani kunbwa kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa za kuhakikisha Watanzania wanapatiwa huduma bora za kibingwa.

    Upandikizaji wa vifaa hivyo utafanywa na timu ya wataalam 10 wa Muhimbili na wataalam wawili kutoka Misri akiwamo Prof. Lobna El Fiky, Mohamed El Disouky.

Ad

Unaweza kuangalia pia

ONGEZENI KASI YA KUWAHUDUMIA WANANCHI – DKT. CHAULA

Watumishi wa afya nchini wametakiwa kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi kwenye vituo vya kutolea huduma …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *