Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji Same-Mwanga-Korogwe

Serikali Imejipanga Kila Eneo – Makamu wa Rais

 • Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema hakuna Maendeleo pasipo Utawala bora.
 • Makamu wa Rais amesema hayo wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mwanga mkoani Kilimanjaro.
 • “Viongozi wa Halmashauri, Viongozi wa Wilaya wasipokuwa na Utawala bora, wasiposhirikiana, Chama, Serikali, Wilaya, Halmashauri tusitegemee kuwa na maendeleo tutalalamika siku zote” alisema Makamu wa Rais.
MAKAMU AKIZUNGUMZA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Cleopa David Msuya (kulia) muda mfupi kabla ya mkutano wa hadhara na wananchi wa Wilaya ya Mwanga. Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Kilimanjaro.
 • Katika ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo Makamu wa Rais alitembelea miradi mbali mbali katika Wilaya ya Same na Mwanga.
 • Akiwa Wilayani Same, Makamu wa Rais aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya New Dawn, Shule ambayo itakuwa ya mchepuo wa masomo ya sayansi na ni maalum kwa Watoto wenye mahitaji maalum na Yatima pamoja na kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa ofisi za Wakala wa Misitu Wilaya ya Same.
MAKAMU WA RAIS AKISALIMIANA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Cleopa David Msuya (kulia) muda mfupi kabla ya mkutano wa hadhara na wananchi wa Wilaya ya Mwanga. Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Kilimanjaro
 • Makamu wa Rais amewahimiza Wakala wa Misitu nchi kuwapa wananchi miche ya kutosha na kuimarisha ulinzi katika hifadhi ya misitu.
 • Akiwa Wilayani Mwanga, Makamu wa Rais aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji Same-Mwanga-Korogwe ambao awamu ya kwanza imekamilika kwa asilimia 76%.
MAMA SAMIA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Clelia Felician wa kampuni ya M.A Kharafi & Sons wakati alipotembelea mradi mkubwa wa maji wa Same – Mwanga – Korogwe ambao awamu ya kwanza imekamilika kwa asilimia 76%.
 • Akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa amesema kwa sasa awamu ya kwanza ambayo ni Miundombinu ya mradi huo imekamilika kwa asilimia 76% na umegharimu bilioni 94.65 ambapo awamu ya pili itakuwa usambazaji wa maji Same na awamu ya tatu itakuwa usambazaji wa maji Mwanga.
SEHEMU YA MIUNDO MBINU
Sehemu ya Miundombinu ya Mradi wa Maji Same-Mwanga-Korogwe ambao asilimia 76% imekamilika.
 • “Serikali imejipanga kila eneo ambalo maji yanapita wananchi watafaidika na maji hayo” alisema Waziri wa Maji.
 • Kwa upande wake Makamu wa Rais alisema Serikali imedhamiria kutatua tatizo la maji nchi na kuwataka wananchi kutambua kuwa miradi hii ya maji ina gharama kubwa hivyo inabidi wawe walinzi wazuri wa miundombinu ya maji.
MAKAMU AKIWEKA JIWE
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji Same-Mwanga-Korogwe
 • Katika ziara hiyo Wilayani Same na Mwanga Makamu wa Rais ameongozana na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Wiliam Lukuvi.
MAKAMU NA WAZIRI MKUU MSTAAFU
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Cleopa David Msuya (kulia) muda mfupi kabla ya mkutano wa hadhara na wananchi wa Wilaya ya Mwanga. Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Kilimanjaro.
Ad

Unaweza kuangalia pia

TANZANIA YATAKA AMANI KUPUNGUZA MZIGO WA WAKIMBIZI AFRIKA

Tanzania imetaka Umoja wa Afrika na Jumuiya za Kimataifa kuongeza jitihada na nguvu katika kuleta …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *