“Njia pekee ya kuwalinda watoto wa Kike ni kuwapeleka shule” – MAKAMU WA RAIS

 • Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  amemaliza ziara yake ya siku 5 mkoani Manyara.
 • Akizungumza kwenye kikao cha majumuisho ambacho kilihudhuriwa na Viongozi na Watendaji wa mkoa huo Makamu wa Rais aliwapongeza kwa kazi nzuri wanayofanya na kuainisha maeneo kadhaa ambayo yanatakiwa kutupiwa jicho.
MAKAMU AKIZUNGUMZA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi na Watendaji wa mkoa wa Manyara wakati wa kikao cha Majumuisho ya ziara yake kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa uliopo Babati mkoani Manyara
 • Baadhi ya maeneo hayo ni Mazingira ambapo aliuambia Uongozi huo kupanda miti ya kutosha, kulinda maeneo yanayochimbwa madini kuwa kuwasimamia wachimbaji katika kutunza mazingira pamoja na kutunza vyanzo vya maji.
 • Eneo jingine alilozungumzia Makamu wa Rais ni suala zima la Lishe bora kwa watoto na kuhamasisha wananchi kuwa na Bima ya Afya.
MAKAMU
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akivaa urembo mkononi ulioshinwa na kuandikwa jina lake.
 • Makamu wa Rais ameutaka Uongozi wa mkoa huo kuliangalia suala la mimba za utotoni ambalo kwa kiasi kikubwa linaupa mkoa sura mbaya ambapo mpaka sasa kwa mujibu wa ripoti zaidi ya watoto 4200 wamepata mimba wakiwa na umri mdogo.
 • “Njia pekee ya kuwalinda watoto wa Kike ni kuwapeleka shule”alisema Makamu wa Rais.
 • Aidha Makamu wa Rais amehimiza umuhimu wa elimu kwa kushirikisha Mabaraza ya Wazee wa Makabila ili kuzuia mila potufu za ukeketaji.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mhe. Flatei Massay mara baada ya kumaliza kikao cha Majumuisho ya ziara yake na Viongozi pamoja na Watendaji wa mkoa huo.
 • “Si rahisi kumuachisha mila yake lakini tukiwaelewesha na kuwaelimisha vizuri taratibu watatuelewa na kuacha kabisa”
 • Makamu wa Rais ameuambia Uongozi wa mkoa huo wafuate miongozo ya kazi “Kazi za Serikali zina Miongozo, Sheria na Kanuni tulizojiwekea”
 • Mwisho, Makamu wa Rais aliushukuru uongozi huo na kuahidi kurudi tena kwenye Wilaya ambazo hakufika.
Makamu wa Rais
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wakazi wa wilaya ya Kondoa wakati akiwa njiani kurudi Dodoma akitokea mkoani Manyara ambapo alikuwa kwenye ziara ya siku tano ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo.
 • Kwa upande mwingine Mkuu wa Mkoa wa Manyara amemshukuru Makamu wa Rais kwa kufanya ziara mkoani humo ambapo alisema ziara hiyo imekuwa na Mafunzo, Ushauri na Maelekezo ambayo wataenda kutakeleza kama walivyoambiwa.
Sehemu ya Viongozi na Watendaji
Sehemu ya Viongozi na Watendaji wa mkoa wa Manyara wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yako mkoani humo.
 • Akiwa njia kuelekea Dodoma, Makamu wa Rais alisimama barabarani na kuwasalimia wananchi wa Kondoa waliojitokeza ambapo aliwaeleza azma ya Serikali ya kuendelea kutekeleza ahadi zake kwa wananchi na kuwapongeza kwa kupata barabara nzuri inayotoka Dodoma mpaka Babati.
MAKAMU WA RAIS AKIMUAGA MKUU WA MKOA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti mara baada ya kumaliza kikao cha Majumuisho ya ziara yake na Viongozi pamoja na Watendaji wa mkoa huo.
Ad

Unaweza kuangalia pia

TANZANIA YATAKA AMANI KUPUNGUZA MZIGO WA WAKIMBIZI AFRIKA

Tanzania imetaka Umoja wa Afrika na Jumuiya za Kimataifa kuongeza jitihada na nguvu katika kuleta …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *