Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyesimama mbele amefunga mikono) akiwa kwenye picha ya pamoja na waalimu wa shule za sekondari, viongozi na watendaji wa mkoa wa Katavi na Manispaa ya Mpanda. Wan ne kulia ni Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi na wa tano kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Abdallah Malela

NAIBU WAZIRI NDITIYE AKABIDHI KOMPYUTA SHULE ZA SEKONDARI MPANDA

  • Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amekabidhi kompyuta 25 kwa shule za sekondari Mpanda mkoani Katavi kwa lengo la kukuza kiwango cha ufaulu na kuongeza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) shuleni kwa kuwawezesha waalimu kutumia kufundishia na wanafunzi kujifunzia.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akifafanua jambo kwa viongozi wa Mkoa wa Katavi, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda na waalimu wa sekondari (hawapo pichani) kuhusu ukuaji na maendeleo wa sekta ya Mawasiliano nchini. Kulia kwake ni Mbunge wa Mpanda Mjini, Mhe. Sebastian Kapufi na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Abdallah Malela.
  • Amefafanua kuwa lengo ni kupate wanafunzi mahiri kwa kompyuta hizo kutumika na wanafunzi wengine kwenye shule mbali mbali kwa kuziunganisha kompyuta hizo kwenye mtandao ili mwalimu mmoja aweze kufundisha wanafunzi wengi wengine wa shule nyingine
  • “Kumbukeni hapo zamani wanafunzi wa mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma ilikuwa inatoa wanafunzi wenye ufaulu mzuri, hivyo tuwarithishe wanafunzi wetu,” amesisitiza Nditiye
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akikabidhi kompyuta kwa Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi (wa pili kulia) kwa ajili ya shule za sekondari mjini humo. Wakishuhudia, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Albert Richard na Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Abdallah Malela (wa pili kushoto)
  • Kompyuta hizo zimetolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ambao una dhamana ya kuhakikisha wananchi waishio vijijini na maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara wana wasiliana kwa kuzipatia kampuni za simu za mkononi ruzuku ya kujenga minara ili kufikisha huduma za mawasiliano maeneo mbali mbali nchini
Waalimu wa shule za sekondari, viongozi na watendaji
Waalimu wa shule za sekondari, viongozi na watendaji wa mkoa wa Katavi na Manispaa ya Mpanda wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) wakati akiwahutubia kabla ya kukabidhi kompyuta kwa ajili ya shule za sekondari za Mpanda.
  • Nditiye amekabidhi kompyuta 25 zenye thamani ya shilingi milioni 46 kwa Mbunge wa Mpanda Mjini, Mhe. Sebastian Kapufi kwa niaba ya waalimu na wanafunzi wa shule za sekondari zilizopo mjini humo kwa kuwa aliiomba Serikali kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu  ili shule hizo ziweze kupatiwa kompyuta hizo.
  • “Nimeanza kumsumbua Nditiye zaidi ya mwaka mmoja na nusu kuomba kompyuta, unaweza kuona kompyuta ni chombo chepesi ila sio hivyo kwa kuwa ni chombo muhimu na kitatunza siri,” amesema Kapufi
Ad

Unaweza kuangalia pia

UKARABATI WA KIVUKO CHA MV. PANGANI II WAKAMILIKA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *