RAIS MAGUFULI ANGARA AFRIKA KWENYE UCHUMI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameendelea kung’ara kimataifa katika mapambano dhidi ya rushwa na utawala bora.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi Jijini Dodoma, wakati akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa masuala mbalimbali ya Serikali.

Ad

“Kutokana na utendaji wa kimageuzi wa Rais Magufuli, licha ya juhudi za watu wachache kuhaha kutaka kuichafua nchi yetu kimataifa, Tanzania imeendelea kuwa na taswira nzuri na heshima kubwa na ikiendelea kukubalika sana miongoni mwa Mataifa mbalimbali” amesema Dkt. Abbas

Dkt. Abbasi amefafanua kuwa, kimataifa Rais Magufuli amekuwa akiipatia heshima kubwa nchi ya Tanzania kwa mapambano yasiyokoma dhidi ya rushwa hivyo taasisi za kimataifa ikiwemo TRANSPARENCY INTERNATIONAL zimeonesha Tanzania inaendelea kufanya vizuri katika miaka hii mitatu ikitoka nafasi ya 117 hadi 99.

Aidha, Dkt. Abbasi ameongeza kuwa, Novemba, 2018 Serikali ya Nigeria ilitoa Tuzo ya Uongozi Bora kwa viongozi mbalimbali duniani akiwemo Rais Magufuli, mara baada ya Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa na Ufundi yaliyofanyika nchini humo.

“Jumla ya washiriki 123,446 walipiga kura kwenye tovuti ya Jarida la ALM kutoka Afrika na sehemu mbalimbali duniani, huku wengine 33,000 wakitumia mitandao ya kijamii na 3,400 wakituma maoni yao kupitia baruapepe na majukwaa mengine hivyo ili kupata ushindi huo. Rais Magufuli aliwashinda viongozi wengine mashuhuri wa Afrika ambao ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha APC, Nigeria, Chifu Bola Ahmed Tinubu, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini na Rais Nana Akufo-Addo wa Ghana”ameeleza Dkt. Abbasi.

Akizunguza kuhusu hali ya uchumi nchini Dkt. Abbasi ameeleza kuwa, Serikali inaamini Mwaka huu 2019 ukuaji wa uchumi nchini utafika asilimia 7.2 na kuifanya Tanzania kuendelea kuwa katika mataifa matano Afrika kwa uchumi unaokua kwa kasi na kuendelea kuwemo katika 10 ya dunia.

“Tanzania imekuwa nchi ya tano barani Afrika katika ukuaji wa uchumi na hii inatokana na utekelezaji wa miradi na huduma mbalimbali za kiuchumi zinazoendelea” amesema Dkt. Abassi.

Mbali na hayo Dkt. Abbasi amesema kuwa Serikali itaendelea kutekeleza kwa kasi wajibu wake kwa umma ikiwemo kuhakikisha hali ya amani, utulivu, kusimamia utawala bora na utawala wa she

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS MAGUFULI AIPONGEZA MAHAKAMA NA WADAU KWA MAFANIKIO MAKUBWA

Rais  Dkt. John  Magufuli ameipongeza Mahakama na wadau wake kwa hatua kubwa za kimaendeleo zilizopigwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *