Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufguli na Mkurugenzi mtendaji African Media Group (AMG) Jaffari Haniu wakimsikiliza mtangazaji wa kituo cha Channel Ten Hanifa Roy alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.

MNA WAJIBU WA KUZUNGUMZIA MAZURI YA TANZANIA – RAIS MAGUFULI

RAIS MAGUFULI
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumzana Wafanyakazi na Watangazaji wa Channel Ten na Radio Magic Fm, alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Bi. Diana Mwakatundu ambaye ni Mlemavu aliwapokuwa akizungumza na Wananchi mbalimbali waliokuwa nje ya Ofisi za Channel Ten na Radio Magic Fm, alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.
 • Rais Dkt. John Magufuli amewahakikishia Watanzania wote kuwa Taifa linakwenda katika mwelekeo mzuri hasa baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha uchumi na huduma za kijamii kama vile afya, elimu, maji, nishati na miundombinu ya usafiri.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi mbalimbali waliokuwa nje ya Ofisi za Channel Ten na Radio Magic Fm, alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.
 • Mhe. Rais Magufuli amesema hay alipokutana na wananchi katika Mtaa wa Zanaki, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kutembelea kampuni ya Africa Media Group (AMGL) yenye vituo vinne vya televisheni ikiwemo channel Ten na vituo viwili vya redio ikiwemo Magic FM, ambayo kwa sasa inamilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Wananchi mbalimbali wakimsikiliza Rais
Wananchi mbalimbali wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliwapokuwa akizungumza nao Wananchi hao waliokuwa nje ya Ofisi za Channel Ten na Radio Magic Fm, alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.
 • Rais Magufuli amesema pamoja na mafanikio hayo, Serikali itaendelea kupambana na dhuluma na matumizi mabaya ya rasilimali za Taifa na ametoa wito kwa Watanzania wote kuiunga mkono kwa kuhakikishia wanatanguliza maslahi ya Taifa.
Mama Janeth Magufuli Mke wa Rais
Mama Janeth Magufuli Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimu Wananchi mbalimbali waliokuwa nje ya Ofisi za Channel Ten na Radio Magic Fm, walipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.
 • Akiwa ndani ya jengo la AMGL, Mhe. Rais ambaye ni Mwenyekiti CCM amejionea mitambo, chumba cha habari na studio za kurushia matangazo za kituo cha redio cha Magic FM na kituo cha televisheni cha Channel Ten, na pia amezungumza na wafanyakazi ambao wamemueleza changamoto mbalimbali zikiwemo uhaba na uchakavu wa vitendea kazi, maslahi madogo ya wafanyakazi na uchakavu wa jengo la kituo hicho.
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth wakimsikiliza mtayarishaji vipindi wa kituo cha Televisheni cha Channel Ten Issa Didi alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.
 • Rais Magufuli ameahidi kutoa shilingi Milioni 200 ndani ya siku 2 kwa ajili ya kununulia vitendea kazi vya kituo hicho na pia amewataka wafanyakazi wa AMGL kumpelekea mapendekezo ya jengo lolote la CCM lenye hadhi nzuri ili kuhamishiwa kituo hicho.
RAIS DR
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mmoja wa Wafanyakzi na Mtangazaji wa Radio Magic Fm Orest Kawawo alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.
 • Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewapongeza wafanyakazi hao kwa kazi nzuri wanazozifanya na amesema kuwa dhamira yake ni kuhakikisha kituo hicho kinaboreshwa, matangazo yake yanafika maeneo mengi ya ndani na nje ya nchi na kinakuwa kituo cha mfano kwa vituo vingine hapa nchini.
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi wa Ufundi wa Channel Ten Agustino Mganga alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.
 • Pia amewataka wafanyakazi hao kujenga umoja wa dhati, kuchapa kazi kwa juhudi zaidi ili kuongeza uzalishaji wa mapato na kuzalisha maudhui ambayo yatawasaidia Watanzania kupata manufaa kama vile kutoa elimu ya kilimo, biashara, ufugaji na uvuvi.
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi mtendaji African Media Group (AMG) Jaffari Haniu alipotembelea ili kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.
 • “Nataka Africa Media Group Ltd iwe na vyombo vyenye nguvu, vinavyotazamwa kila mahali hapa nchini hadi nje ya nchi, Tanzania haiwezi kuwa soko la kuangalia vyombo vya habari vya kutoka nje ya nchi, watu waangalie vyombo vya habari vya nje lakini vyombo vyetu viwe ndio mwongozo wa maisha ya Watanzania zaidi ya Milioni 50.
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth katika chumba cha kurushia matangazo cha Rdio Magic Fm alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM.
 • “Na hii natoa wito kwa vyombo vyote vya Tanzania, mna wajibu wa kuzungumzia mazuri ya Tanzania, lakini pia muendelee kutoa elimu kwa Watanzania, Watanzania karibu asilimia 75 ni wakulima, toeni vipindi vya kuonesha kilimo bora, ufugaji bora, nakadhalika” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika chumba cha kusomea Habari cha kituo cha Televisheni cha Channel Ten alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.
 • Baada ya kutoka AMGL, Mhe. Rais Magufuli amekagua mradi wa ukarabati mkubwa wa jengo la kitega uchumi la CCM (SUKITA) lililopo mtaa wa Lumumba Jijini Dar es Salaam ambalo litakamilika mwezi Juni mwaka huu, na akiwa nje ya jengo hilo amesalimiana na wananchi wakiwemo wafanyabiashara ndogondogo ambao amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kutimiza wajibu wake wa kuwapigania Watanzania wote bila kubagua.
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi mtendaji African Media Group (AMG) Jaffari Haniu akisoma habari, alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.
 • Rais Magufuli amemalizia ziara yake kwa kutembelea Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba Jijini Dar es Salaam na kuzungumza na wafanyakazi ambapo amewahakikishia kuwa chama chao (ambacho ni chama tawala) kinakwenda vizuri hasa baada ya hatua zilizochukuliwa kusimamia misingi ya chama, mali na mapato ya chama, maadili na uongozi na pia kurejesha mali za chama zilizokuwa mbioni kupotea.

 

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS MAGUFULI ATEMBELEA DAR ES SALAAM ZOO, AVUTIWA NA WANYAMA WENGI WANAOFUGWA HUMO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *