SERIKALI YATENGA TRIL 3 KUMALIZA MIRADI YA MAJI MIJINI NA VIJIJINI

  • Serikali imetenga zaidi ya sh Tril. 3 kwa ajili ya miradi ya maji mijini na vijijini ili kuhakikisha tatizo la maji linamalizika kabisa nchini. Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Kitila Mkumbo amesema hadi sasa miradi mikubwa 477 inatekelezwa vijijini huku 71 ikiwa mijini na mpaka sasa tayari mradi 71 imekamilika kwa vijijini.
  • Mkumbo amesema,  mwaka 2015 wakati serikali ikiingia madarakani hali ya upatikanaji wa maji vijijini ilikuwa asilimia 53 lakini hadi kufikia Desemba mwaka jana hali ya upatikanaji wa maji imeongezeka na kufika asilimia 59, huku upande wa mijini kwa awamu Hizo, upatikanaji wa maji umeongezeka kutoka asilimia 68 mpaka asilimia 78,
  • Akiongelea kuhusu miradi mbalimbalii ya maji inayoendelea kutekelezwa na serikali,  Mkumbo amesema, katika kuhakikisha wanamaliza matatizo hayo hasa kwa miaka iliyoko juu mfano Kanda ya Ziwa wanategemea kuchukua maji kutoka Ziwa Victoria ambapo miradi 17 itatumia maji kutoka ziwa hilo na zimetengwa Sh. Bilioni 788 kukamilisha hilo.
  • “Hadi sasa tayari kuna vituo 123,000 vyenye uwezo wa kuhudumia wananchi asilimia 85 kama vingefanya kazi lakini kwasababu havifanyi kazi kwasasa vinauwezo wa kuhudumia asilimia 59 tu ya watu,” amesma.
  • Aidha ameongeza kuwa, katika kudhibiti matumizi mabaya ya miradi ya maji, wameshapeleka muswada wa sheria ya majisafi na mazingira ambao utasaidia mambo mengi ikiwemo kuanzishwa kwa wakala wa maji vijijini (Ruwasa), pia utatoa maelekezo ya wasimamizi wa miradi hiyo, kuwaadhibu watendaji wasio waadilifu na wameongeza adhabu kwa waharibifu wa miundombinu.
  • Aidha katika kudhibiti upotevu wa maji ambapo kwasasa umefikia asilimia 40 katika jiji la Dar es Salaam, wanafanya ukarabati wa miundombinu ambapo Dola za kimarekani Mil. 20 zimetengwa ambapo watafumua mabomba ya mchina ambayo utafiti mdogo umeonyesha hayana nguvu ya kuhimili msukumo wa maji yanayotoka kwasasa.
  • “Mradi huu utatekelezwa kwa kipindi cha miezi sita mpaka mwaka. Na pia tupo kwenye mchakato wa kununua mtambo mpya wa kudhibiti maji,” ameongeza Mkumbo
  • Ameongeza katika wizara hiyo wanakabiliana na changamoto mbali mbali Kwani,  mahitaji ni makubwa kuliko rasilimali zilizopo.Na Karama Kenyunko
Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: RAIS DKT. MAGUFULI AKIWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUA HIVI KARIBUNI. IKULU JIJINI DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli awaapisha Viongozi aliowateua hivi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *