WAZALISHAJI SUKARI NCHINI WATAKIWA KUONGEZA UZALISHAJI

  • Serikali imesema kuanzia sasa haitatoa vibali vya uagizaji sukari nje ya nchi kwa wazalishaji wa sukari badala yake serikali itatafuta utaratibu mwingine wa kuagiza.
  • Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga ameyasema hayo wakati akifungua mkutano na Wadau wa Sekta Binafsi ambapo; lengo lilikuwa ni kubadilishana uzoefu, kupata maoni yao namna bora ya kuongeza mahusiano pamoja na utekelezaji wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP II) ambayo inatekelezwa kwa pamoja kati ya Serikali na Sekta Binafsi.

SUKARI

  • Waziri Hasunga amewataka wazalishaji hao wa sukari nchini kuja na mkakati wa namnagani wataongeza uzalishaji ili Tanzania iondoke na hitaji la kuagiza bidhaa hiyo nje ya nchi.
  • Waziri Hasunga amesema kwa kuwapa vibali vya kuagiza nje wazalishaji wa ndani hawataongeza uzalishaji ili waendelee kuagiza nje kwa kuwa sukari ya kutoka nje ni bei nafuu.
  • Amesema mahitaji la sukari kwa mwaka ni Tani 670,000 wakati inayozalishwa na viwanda vya ndani Tani 320,000 na kuwaagiza Wazalishaji hao badala ya kutafuta vibali
    vya kuagiza sukari nje ya nchi waje na mkakati wa kuboresha zaidi uhitaji uliopo kwani Tanzania ina ardhi nzuri pamoja na mashamba ya kutosha.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MINADA 6 YA KOROSHO MSIMU WA MWAKA 2019/2020 YAINGIZA BILIONI 406.3

Zao la korosho katika msimu wa kilimo wa mwaka 2019/2020 limeingiza zaidi ya Bilioni 406.3 …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *